RC Mnyeti, Mbunge Ole Milya waitwa TAKUKURU

Status
Not open for further replies.

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Rc Mnyeti, Mbunge Ole Milya waitwa Takukuru

Mwandishi wetu, Manyara

Siku chache baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya na mkuu wa mkoa huo kushutumiana kwa rushwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imewaita ofisini.

Ole Milya na Mnyeti walishutumiana hivi Karibuni mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya migogoro ya mipaka baina ya Tanzanite One na wachimbaji wadogo.

Katika shutuma hizo Ole Milya alimtuhumu hadharani Mnyeti kupokea rushwa kutoka kampuni ya Tanzanite One kwa lengo la kuwakandamiza wachimbaji wadogo huku akihoji ukaribu wa kiongozi huyo na wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Hatahivyo, Mnyeti naye alimtuhumu Ole Milya kuwatishia kwa silaha ya moto (bastola) baadhi ya wafanyabiashara wa madini mkoani humo huku akienda mbali na kudai kwamba ana kesi tano ambazo zimewasilishwa mezani kwake zinazomhusu.

Taarifa kutoka Takukuru zinadai kwamba viongozi hao wameitwa mnamo Agosti 6 mwaka huu katika ofisi za Takukuru mkoani Manyara ili waweze kutoa maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo.

Hatahivyo taarifa zinadai kwamba tayari mkuu wa wilaya ya Simanjiro mkoani humo, Zephaniah Chaula ameanza kuwapigia simu baadhi ya wafanyabiashara kwa agizo la Mnyeti ili wajitokeze mbele ya Takukuru kutoa maelezo kwamba walitishiwa silaha na Ole Milya.

Hatahivyo, Takukuru pia inachunguza taarifa kuhusu utajiri wa Rc Mnyeti aliojipatia ghafla akiwa mkuu wa mkoa wa Manyara na endapo mali hizo ameziorodhesha Serikalini katika orodha ya mali anazomiliki.

Miongoni mwa mali hizo ni hoteli ya kitalii anayojenga kanda ya ziwa, shule ya sekondari, klabu ya soka ya Gwambina FCpamoja na mabasi mbalimbali ya kusafirisha abiria.

Mwisho.

======

UPDATES: 4 AUG 2019, 1740HRS

KANUSHO;

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Fidelis Karungura, amekanusha habari hii. Amesema Taarifa Zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya na mkuu wa mkoa huo amheshimiwa Mnyeti, zonafanyiwa kazi kwa umakini Mkubwa. Na Kama itahitajika kuwaita, watafanya hivyo ili wawape taarifa zaidi. Ila hadi muda huu bado hawajawaita.
IMG-20190728-WA0025.jpeg
 
Mnyeti anajitetea kitoto sana. Eti kesi tano za kutishia kwa silaha zipo mezani kwake as if ofisi take Ina counter ya polisi au masjala ya mahakama!

Hii awamu imepatwa kuliko jua kwa kuteuliwa viongozi walio na Giza ubongoni mwao kuwaongoza wenzao nuruni. Aliyewateua naye anawachekea tu!

Yetu macho na masikio na tunasubiri mapambio ya sifa kutoka takukuru kuwasafisha ccm waliojichafua kwa bahati mbaya! Ikiwapendeza wamkumbushe kwa kumwonyesha zile video za dogojanja!
 
Huyu alikuwa mwalimu tu, Leo mnyeti ni bilionea kuna harufu kubwa ya ufisadi. Haiwezekani ukuu wa mkoa kwa miaka 3 tu haiwezekani
 
Huyo Mnyeti ni mla rushwa wa waziwazi na analindwa na mkulu. Alipandishwa cheo baada ya kutembeza rushwa kwa madiwani wa cdm huko Arusha. Wakati ule mkulu aliamua kufumbia macho rushwa ile, kwa sababu hata yeye anapambana na rushwa kwa misingi ya itikadi na sio upambanaji wa kweli wa rushwa. Na huu uminywaji wa vyombo vya habari kutokuripoti maovu ya watu wa serikali, kumechangia sana rushwa kushamiri kwani watendaji wa serikali wamejuwa wako salama kwakuwa maovu yao hayatatangazwa.

Hata hivyo suala hilo limefika mbele kwakuwa Ole Millya sasa ni mbunge wa ccm, lakini angetoa tuhuma hizo akiwa mbunge wa cdm suala hilo lingewekwa siasa, kwani hakuna vita yoyote halisi ya rushwa zaidi ya kiki za kisiasa. Ukweli ni kuwa hatua za rushwa zitachukuliwa dhidi ya mla rushwa asiyemsujudia rais ili kuhadaa umma kwamba kuna vita ya rushwa. Na hata huyo Mnyeti hatachukuliwa hatua yoyote zaidi ya maelewano ya nyuma ya pazia, kwani amefika kwenye cheo hicho kwa kufuata maelekezo ya mkulu kutekeleza rushwa ya ununuzi wa madiwani. Ogopa sana mtu anayesema anapambana na rushwa kisha hataki uwazi.
 
Rc Mnyeti, Mbunge Ole Milya waitwa Takukuru

Mwandishi wetu, Manyara

Siku chache baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya na mkuu wa mkoa huo kushutumiana kwa rushwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imewaita ofisini.

Ole Milya na Mnyeti walishutumiana hivi Karibuni mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya migogoro ya mipaka baina ya Tanzanite One na wachimbaji wadogo.

Katika shutuma hizo Ole Milya alimtuhumu hadharani Mnyeti kupokea rushwa kutoka kampuni ya Tanzanite One kwa lengo la kuwakandamiza wachimbaji wadogo huku akihoji ukaribu wa kiongozi huyo na wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Hatahivyo, Mnyeti naye alimtuhumu Ole Milya kuwatishia kwa silaha ya moto (bastola) baadhi ya wafanyabiashara wa madini mkoani humo huku akienda mbali na kudai kwamba ana kesi tano ambazo zimewasilishwa mezani kwake zinazomhusu.

Taarifa kutoka Takukuru zinadai kwamba viongozi hao wameitwa mnamo Agosti 6 mwaka huu katika ofisi za Takukuru mkoani Manyara ili waweze kutoa maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo.

Hatahivyo taarifa zinadai kwamba tayari mkuu wa wilaya ya Simanjiro mkoani humo, Zephaniah Chaula ameanza kuwapigia simu baadhi ya wafanyabiashara kwa agizo la Mnyeti ili wajitokeze mbele ya Takukuru kutoa maelezo kwamba walitishiwa silaha na Ole Milya.

Hatahivyo, Takukuru pia inachunguza taarifa kuhusu utajiri wa Rc Mnyeti aliojipatia ghafla akiwa mkuu wa mkoa wa Manyara na endapo mali hizo ameziorodhesha Serikalini katika orodha ya mali anazomiliki.

Miongoni mwa mali hizo ni hoteli ya kitalii anayojenga kanda ya ziwa, shule ya sekondari, klabu ya soka ya Gwambina FCpamoja na mabasi mbalimbali ya kusafirisha abiria.

Mwisho. View attachment 1171728

Uaneni
 
Kule Ikulu waliona 1.5trilion zilivyoyayuka,na wao wanatengeneza miyayusho yao,role model wanae,uhalali wa kutenda hayo ni kuwanyanyasa wapinzani!!
 
Naomba nipewe ukuu wa wilaya jamani ili niwatumikie wananchi kwa uadilifu.
Sio vizuri kula jasho la wengine
 
Wameitwa kwenda kutembelea ofisi za takukuru hao, tuhuma za mtoa rushwa na mpokea rushwa wa CCM hazijawahi kuwa kesi hata siku moja zinaishia kuwa tuhuma hivyohivyo, sanasana wakijitahidi watapelekwa mahakamani kwa kufunika kombe mwanaharamu apite. baada ya hapo ni CCM hoyee kwa kwenda mbele.
 
Hahaha Ole Millya anadhani bado yuko CHADEMA. Au kapeleka vita ndani?!
Kule CCM utaratibu ni kukaa kimya wakati wa kula, kuongea wakati wa kula kunamfanya abaki na njaa.
 
Hii itakuwa mara ya pili anatuhumiwa kwa rushwa. Naona hawa wanatumiwa mgongo wa kuaminiwa na Rais kufisadi nchi maana kutokana na utendaji wao wanona hata wakishutumiwa itaonekana ni majungu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom