RC Mnyeti atengua agizo la Kigwangalla la kuwataka wakazi wa Kimotoro mkoani Manyara kuhama eneo la hifadhi

sasa sisi tufanyaje? nchi inaendeshwa kihuni haijulikani dereva ni nani na mpiga debe ni nani, mmehiaribu sana hii nchi. yaani watanzania hapa tulikosea sana Mungu atusamehe

Mmmh
Mimi ningekuwa abiria wake basi mngeisoma namba na kutii sheria haswaa.. acha uvivu na kulalamika amka utende yako.. huoni aibu kuisingizia serikali kwa yako unayopitia!!
 
Kambale at work!
Nani mkubwa nani mdogo haijulikani.

Na kule bukoba natamani na wengine aseme mitumbwi isizamishwe
 
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu wa mkoa wa Manyara ametengua agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii la kutaka wakazi wa Kimontorok mkoan Manyara kuhama eneo la hifadhi.

Chanzo: Azam news
Inawezekana sisi Kwa nje,tunaona kama ametengua kauli ya waziri,lkn pengine walipanga wote wafanye sinema ili wapate sifa za kisiasa
 
Tamko la Waziri wa Maliasili na Utalii Dakta Hamisi Kigwangala la kuwataka Wananchi wa Kaya takribani elfu tatu katika Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro wahame kupisha shughuli za uhifadhi limeonekana kukinzana na Maamuzi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexsander Mnyeti ambaye ametoa zuio la wakazi hao kuondoka kwa sasa.



Chanzo: Azam Tv
 
Hapa hakuna mkubwa kwa kigezo kuwa wote ni Wateule wa Raisi lakini tukiangalia uhalisia Waziri ni mkubwa kuliko Mkuu wa Mkoa kwanza ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri
 
Back
Top Bottom