RC Mnyeti atengua agizo la Kigwangalla la kuwataka wakazi wa Kimotoro mkoani Manyara kuhama eneo la hifadhi

byembalilwa

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
2,032
917
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametengua agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla la kutaka wakazi wa kaya 3000 wa kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kuhama eneo la hifadhi.

Kigwangala alitoa alitoa miezi 9 mnamo Februari 23 mwaka huu kwa wananchi wawe wameondoka eneo hilo

Mnyeti amesema wananchi wasubiri hadi wataalamu wa ardhi watakapokuja kusema mipaka halali kati ya makazi ya watu na hifadhi



Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametengua agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyewapa miezi tisa wananchi wa Kijiji cha Kimotorok kuondoka katika maeneo wanayoishi wakidaiwa kuvamia Hifadhi ya Tarangire wilayani Simanjiro.

Akizungumza na wanakijiji hao juzi, Mnyeti alisema hakuna atakayekwenda kuwafukuza na kama hilo lipo, yeye ndiye atawaambia wanafukuzwa au la, hivyo wawe na amani.

Mnyeti alisema ofisi ya mkoa inajiandaa kutuma wataalamu kwenda kupima eneo hilo ili kutatua mgogoro.

Februari 25, Waziri Kigwangalla aliwapa wananchi wa kijiji hicho, vitongoji vya Massas na Loon’benek miezi tisa wawe wamehama kwa kuwa wamevamia eneo la Hifadhi ya Tarangire.

Baadaye alitoa ufafanuzi akisema kabla ya kuondoka, Serikali itawalipa fidia na watatafutiwa maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kujengewa zahanati nje ya hifadhi kutokana na iliyokuwapo kuwa ndani.

Dk Kigwangalla alipotafutwa jana kuzungumzia kauli ya Mnyeti alisema, “Sijapata taarifa rasmi kwa maandishi. Siwezi kufanyia kazi taarifa za kwenye mitandao. Nitasubiri barua kama itakuja. Hata hivyo, sina hakika kama mkuu wa mkoa anaweza kusema hivyo.”

Mkuu wa mkoa Mnyeti alitoa kauli baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi wa Kimotorok alipokuwa akienda kwenye mkutano wa kuwapokea wanachama zaidi ya 3,000 wa CCM kutoka vyama vingine.

Wananchi wa Kimotorok

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Saringo ole Meeki alimuomba mkuu wa mkoa kuwasimamia katika kupata haki ya ardhi yao wanayotaka kuporwa na watu wa hifadhi bila hata kuwashirikisha kwa lolote juu ya jambo wanalolifanya ikiwamo kuweka alama (bikoni) ndani ya ardhi ya kijiji hicho ambacho kina hatimiliki tangu miaka ya 1970.

“Bikoni zimewekwa hapa hivi karibuni chini ya ulinzi mkali tukiwa hata hatuelewi na baadhi yetu waliouliza walijibiwa ‘hatuna nafasi ya kuongea na mtu yeyote’ lakini baada ya kufuatilia kwa undani ndipo tukagundua wanasema ni mchoro wa eneo la hifadhi,” alisema Meeki.

Alisema, “Mheshimiwa jambo hili limefanywa kinyume cha utaratibu kwa kuwa mbali na kutoshirikishwa kwenye uwekaji wa bikoni lakini pia hatukuulizwa juu ya upitishwaji michoro ya makubaliano ya mipaka ya kijiji na hifadhi kwa kuwa alama mpya zimesogezwa na zimemega vitongoji viwili.”

Mkazi mwingine, Baby Noah alisema mbali ya alama kuwekwa kwenye maeneo yao, agizo la waziri wa maliasili la kuwapa miezi tisa kuhama limewaathiri.

“Mkuu tusaidie kutatua mgogoro huu maana hapa ni kwetu na hatujui pa kwenda, hivyo hatutakubali kuhama maana tuko hapa kwa miaka mingi na kijiji kilipata hati miaka ya 1970 lakini mwaka huu tunakuja kuwekewa bikoni eti ni maeneo ya hifadhi kitu ambacho hakiingii akilini,” alisema.

Majibu ya Mnyeti

Akijibu hoja za wananchi, Mnyeti aliomba apewe siku 10 awe amefanya utaratibu wa kupeleka wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao wako katikati ya wananchi na hifadhi hivyo hawatapendelea upande wowote.

“Sasa chagueni kamati ndogo au Serikali ya kijiji watakaokwenda na wataalamu kukagua alama za mipaka. Watapitia mipaka yote kujua ramani maana hifadhi nayo ina umuhimu wake, hivyo muwe tayari kukubaliana na majibu yatakayosomwa na mtaalamu baada ya ukaguzi maana hata ofisi ya ardhi mkoa haijui utekelezaji wa uwekaji alama hizo,” alisema Mnyeti.

Alisema, “Lakini pia inawezekana mko sahihi maana tunajua hawa watu wa hifadhi mara nyingi wao wanataka kusogeza tu eneo, kila siku wanataka eneo liongezeke, leo anaweza akaja akaishia hapa kesho akija anaishia hapa, sasa tunaleta mtu ambaye yuko katikati ya hifadhi na wananchi na atapima kuleta ukweli.”

Chanzo: Mwananchi
 
kitu gani sio cha kawaida hapo? awamu hii haina coordination,ipo hovyohovyo halafu mnyeti na bashite ni special case,si mnasikia anavyotoaga kauli za kibaguzi kwa chadema na hafanywi kitu?kununua madiwani camera ikamnasa hafanywi kitu,kuna siku hawa na bashite watapiga hata mawaziri vibao

Mwisho wao 2025,yule mbabe alokuwa AR akaenda MZ na kumpigia sm kichaa sisonje kuwa mkurugenzi kamtukana na fyatu sisonje kamfukuza mkurugenzi sasa nae yuko wapi(MULONGO) hata road haonekani
 
Mkuu wa Mkoa lazima atakuwa amepata maelekezo kutoka kwa Mkuu kwa sababu hawezi kwenda kinyume na mjumbe wa mhimili mkuu wa nchi, serikali Kuu. Sasa Je Mkuu hajafurahishwa na kauli ya Kigangwallah dhidi ya nchi jirani kututesea watanzania wenzetu? Ukiwa na ufikiri utagundua kitu. Siku za Kigwangallah zinahesabika nahisi anatamani hata leo amtumbue ila itaonekana ni kwa sababu ya nchi jirani kwa hiyo ngoja atafutiwe sababu nyingine
 
Mkuu wa Mkoa lazima atakuwa amepata maelekezo kutoka kwa Mkuu kwa sababu hawezi kwenda kinyume na mjumbe wa mhimili mkuu wa nchi, serikali Kuu. Sasa Je Mkuu hajafurahishw ana kauli ya Kigangwallah dhidi ya nchi jirani kututesea watanzania wenzetu? Ukiwa na ufikiri utagundua kitu. Siku za Kigwangallah zinahesabika nahisi anatamani hata leo amtumbue ila itaonekana ni kwa sababu ya nchi jirani kwa hiyo ngoja atafutiww nyingine
kweli mkuu
 
Mapacha watatu: mnyeti,gambo,bashite. Hawa ukiwagusa lazima uende na maji. Nape anaujua muziki wa bashite, Nasary anaujua muziki wa mnyeti ashukuru mbwa alimuokoa, yule aliyekuwa mkuu wa mkoa wa arusha kabla ya Gambo pamoja na kujifanya mzee wa kitengo bado alitumbuliwa..Hao wanaitwa the choosen one..gusa unase!.
 
kitu gani sio cha kawaida hapo? awamu hii haina coordination,ipo hovyohovyo halafu mnyeti na bashite ni special case,si mnasikia anavyotoaga kauli za kibaguzi kwa chadema na hafanywi kitu?kununua madiwani camera ikamnasa hafanywi kitu,kuna siku hawa na bashite watapiga hata mawaziri vibao
Halagu Rc ni mtoto wa Baba mwenye nyumba. Atafanywa nini?? Kuonyeshana umwamba..
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom