RC, Mkurugenzi na Meya wa Mwanza, mmeshindwa kuweka taa za barabarani kwenye hili jiji

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Asalaam:

Nimeandika kwa maskitiko makubwa sana

Kwa niaba ya wakazi wote wa jiji la mwanza na vitongoji vyake, ningependa kutoa malalamiko yangu kwa uongozi wote wa jiji la Mwanza

Mwanza ni jiji pendwa hana hapa Tz & East Africa baada ya Dar

Mwanza ndio Second City hapa Tz way back , najua kwa point hii wale jamaa zetu wanao battle na jiji hili watanipinga lakini ukweli utabaki pale pale kwamba
Mwanza ni Second City

Mwanza ndio business hurb ya lake zone & East Africa country

Ni mji maridhawa na wenye mandhali ya kuvutia na watu wake wakarimu sana

Kwa sasa ni jiji lenye miradi mingi mikubwa ya kimkakati inayoendelea

Kero kubwa ya jiji hili ni barabara zake kutokuwa na taa za barabarani zinazosaidia kupunguza uhalifu na ndio kilichopelekea kuandika huu uzi na kuulaumu uongozi wa halmashaur ya jiji la Mwanza

Viongozi mtueleze mnakwama wapi wakati karibu mikoa yote Tz ina taa za barabarani za kuzuia uhalifu?

Mtuwekee taa jamani zinazoendana na hadhi ya jiji hili pendwa tumechoka kutembea kwa mashakamashaka mjini hapa

Kama mnaona hamfit kwenye hizo nafas zenu mlizokaa, wapisheni wapisheni wanaoweza kututatulia hizo changamoto wakae maana tumeshapaza sana sauti mpaka makoo yanakauka

Taa zipo nchi nzima kwanini iwe Mwanza pekee?

Tunataka viongozi wapenda maendeleo sisi.
 
Naunga mkono hoja.hata taa zilizopo nyingi aziwaki zimeharibika.

Taa za kupanda Bugando hospital kuna ambazo aziwaki.
Mtaa wa Nata kuanzia kona ya msikiti wa Ismailia kwenda mpaka mlango mmoja akuna taa.
Kule nyuma ya benki ya damu bugando kunanzia apartment za jeshini kwenda mpaka kona ya Igogo barabara ya mawe kuelekea mpaka hospitali ya Hindu akuna taa kabisa.

Mtaa wa hospitali ya Sekou Tuore kuanzia geti la ofisi ya Almashauri mpaka kuelekea mwisho wa ukuta wa Lake Secondary ule mtaa taa zipo lakini aziwaki.

Barabara ya kutoka Nyegezi stendi kwenda mjini taa zipo lakini aziwaki watengeneze taa ziwake.

Kuanzia makutano ta Pamba road na Kenyata Road kuja Sahara mpaka Nyerere. road kuna taa aziwaki zimezima.

Kingine cha ziada waweke vyombo vya kutupia taka(dust bean)kwenye mitaa ya jiji la Mwanza.
 
Mwanza mwanza mwanza.

Beautiful city on the shores of lake Victoria(Nyanza)

#MaendeleoHayanaChama
 
Naunga mkono hoja.hata taa zilizopo nyingi aziwaki zimeharibika.

Taa za kupanda Bugando hospital kuna ambazo aziwaki.
Mtaa wa Nata kuanzia kona ya msikiti wa Ismailia kwenda mpaka mlango mmoja akuna taa.
Kule nyuma ya benki ya damu bugando kunanzia apartment za jeshini kwenda mpaka kona ya Igogo barabara ya mawe kuelekea mpaka hospitali ya Hindu akuna taa kabisa.

Mtaa wa hospitali ya Sekou Tuore kuanzia geti la ofisi ya Almashauri mpaka kuelekea mwisho wa ukuta wa Lake Secondary ule mtaa taa zipo lakini aziwaki.

Barabara ya kutoka Nyegezi stendi kwenda mjini taa zipo lakini aziwaki watengeneze taa ziwake.

Kuanzia makutano ta Pamba road na Kenyata Road kuja Sahara mpaka Nyerere. road kuna taa aziwaki zimezima.

Kingine cha ziada waweke vyombo vya kutupia taka(dust bean)kwenye mitaa ya jiji la Mwanza.
Bruh usitake kuniambia kuna RC, DC, meya, watendaji wote wa serekali na hawaoni hivo vitu
 
Back
Top Bottom