RC Mjema alalamika viwanda Shinyanga kushindwa kufanya kazi kwa kukosa umeme

kifimbo5

Member
Jun 27, 2022
10
6
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amesema katika Mkoa wa Shinyanga bado kuna tatizo la ukosefu wa huduma ya umeme wa uhakika hasa katika maeneo ya viwanda na migodi hali inayosababisha baadhi ya viwanda kushindwa kufanya kazi na wengine kuzalisha bidhaa kwa zamu sababu umeme haujitoshelezi.

Mjema ametoa malalamiko hayo mbele ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba aliyekuwa ziarani Mkoa wa Shinyanga ambapo Mjema tatizo hilo limesababisha viwanda mkoani humo kushindwa kufanya kazi na wengine kuzalisha bidhaa kwa zamu sababu umeme haujitoshelezi

Amesema bado pia kuna tatizo la usambazwaji wa nguzo za umeme ambapo zoezi lake limekuwa la kusuasua na kuomba huduma hiyo ya umeme iboreshwe haraka ili wananchi wapate huduma ya umeme na wa uhakika na kukuza uchumi wanchi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, naye ametoa malalamiko kwa Shirika la umeme Tanzania TANESCO, kuacha tabia ya urasimu hasa kwenye uunganishaji huduma ya umeme kwa wananchi, ambapo wamekuwa wakichukua muda mrefu licha ya kumaliza kulipia gharama zote.

MJEMA (1).JPG
VIONGOZI 3.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom