RC Mghwira: Nashtakiwa sana kwa Rais Magufuli

Tutanota

Member
Aug 5, 2020
18
77
WAFANYABIASHARA MOSHI WAMSHANGAA RC MGWIRA KUMLAUMU RAIS MAGUFULI

Wafanyabiashara wa manispaa ya Moshi waliokuwa na kikao na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwira wameonesha kushangazwa na Kitendo cha Mkuu huyo kumlaumu hadharani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu kuwa huwa anamshtaki kwa Rais Magufuli juu ya mambo mbalimbali.

Wafanyabiashara hao wametoa maoni yao kupitia Nungwi Fm kwa (sharti la kutotaka majina yao yaandikwe) baada ya kutoka kwenye Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha Mkoa huo,akiongea kwaniaba ya wenzake Mfanyabiashara wa Kwanza alisema "Sisi tulikuja kuona namna gani kero yetu inatatuliwa kwa njia za amani lakini cha kustaajabisha ni kitendo cha RC kumshambulia Meya mbele yetu katika mambo yao ya siri akijua wazi sisi ni raia hatupaswi kusikia mambo yao,tunachoitaji kuona ni mshikamano ili Wafanyabiashara tupate ahueni kwenye maisha yetu" mwisho wa kunukuu

Pia Mfanyabishara mwingine alisema "Meya na RC wote ni watumishi wetu tunategemea wafanye kazi kwa muunganiko sio malumbano haya,Meya amefanya mazuri mengi nahata hili letu amelibeba sana, Kumgombeza na kumfukoe mbele yetu sio Sahihi ,wangesubiri tuondoke wafanye wao kwa wao,hili limetujengea picha mbay vichwani mwetu ,Tunaloomba ni watusikilize Jambo letu hili"


Source : Nungwi Online Fm
 
Kwa kauli za huyu mama kuhusu corona juzi kwenye mazishi ya katibu mkuu wa kkkt dk, nilitegemea figisu kama hizi. Kama huyo mama alimtuhumu meya bila kificho na kama wafanyabiashara wanaona kuwa huyo mama kakosea, kwanini wanaficha majina yao?
Unafiki tu ndio umewajaa. Uoga mpaka kwenye hoja za msingi. Walichoongea ni maswala ya msingi, sijui kwanini wafiche majina yao. Heri huyo mkuu wa mkoa katoa ya moyoni mwake kwao, kuliko wao wanaojificha.

Zao la nchi ya wananchi waoga tu. Tutafika kweli!
 
Unafiki tu ndio umewajaa. Uoga mpaka kwenye hoja za msingi. Walichoongea ni maswala ya msingi, sijui kwanini wafiche majina yao. Heri huyo mkuu wa mkoa katoa ya moyoni mwake kwao, kuliko wao wanaojificha.

Zao la nchi ya wananchi waoga tu. Tutafika kweli!
Ajabu wanashangaa RC kumgombeza Meya wakati huo huo ndio huwa wanampongeza magufuli anapokuwa anawakemea viongozi hadi kuwatumbua hadharani wakisema kuwa wakati wa kuoneana aibu umepita
 
Kwa kauli za huyu mama kuhusu corona juzi kwenye mazishi ya katibu mkuu wa kkkt dk, nilitegemea figisu kama hizi. Kama huyo mama alimtuhumu meya bila kificho na kama wafanyabiashara wanaona kuwa huyo mama kakosea, kwanini wanaficha majina yao?
Wafanyabiashara kama wanasema kweli kwa nini wanaficha majina yao na njia aliyotumia RC kumtuhumu Meya mbele yao, mbona ni njia hiyohiyo anatumia Rais kuwatuhumu wateuliwa wake na kuwatengua mbele ya Watanzania wote? Kumfurahisha Magufuli anayedai hakuna Corona kumbe ipo kibao, Meya huyu si ndo yule aliyeamuru Wajumbe wa Baraza la Madiwani wavue Barakoa walizovaa kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya gonjwa hatari la Corona? Wakati umefika Watanzania kuambiana ukweli bila kujali maslahi!
 
Hizo kazi zisizokuwa na qualification ndio hayo madhara yake, watu wanaona kujipendekeza kulikopitiliza kwa bosi wao ndio kama sifa kwao ya utendaji kazi mzuri, mbaya zaidi unapokuta mwanaume ndio anakuwa na kiherehere zaidi ya mwanamke.

Hapa niko upande wa RC namfahamu yule mama na misimamo yake naielewa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom