RC Mghwira: TRA acheni kufanya kazi kama polisi Wafanyabiashara siyo majambazi, mbunge asema kuwa tajiri imekuwa dhambi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,768
141,632
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dr Mghwira amewatataka TRA kuacha kukusanya kodi kama polisi bali wazingatie dhana ya Huduma kwa mteja ( Customer Care) yaani kumjali mteja.

Mghwira amesema wafanyabiashara siyo majambazi na siyo jambo jema kuwaona wakifunga biashara kila siku.

Naye mbunge wa Hai mh Mafue amewataka TRA kuondoa fikra walizonazo kuwa wafanyabiashara ni kama maadui zao kwa sababu mtu kuwa tajiri siyo dhambi.

Mafue anahoji kama mtaendelea kuwaminya namna hii wafanyabiashara mnadhani huko mbele kodi mtakusanya wapi kwa sababu hawa wote hawatakuwepo.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
TRA endeleeni na kazi, msikatishwe tamaa.

Kilimanjaro kuna mipaka na nchi jirani na panya road chungu mbovu.

Magendo ni mengi kuanzia nyuzi za nguo, simu, sabuni , sukari, mafuta kula, taa etc.

Bila TRA imara tutasomeshwa namba, wafanyabiashara kilimanjaro baadhi ni wakwepakodi wakubwa, TRA uchumi wetu unawategemea msitetereke.
 
Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Ushauri mzuri!
 
..huyu mama asipoangalia atatumbuliwa.

..labda kwasababu ni mweupe basi anajiona yuko salama.
 
Badala kumlenga Muhusika mnawalenga wasio husika....tangu lini Mbwa akamsikiliza Mgeni?, ongeeni na Mwenye Mbwa awaambie Mbwa wake watulie.
 
Safi Sana mama MGWIRA.
TRA akili zao sjui wanafikiriaga kwa kutumia Nini.

Afu
Kule HAI DC ole sabaya nae amegeuka afisa wa TRA.
 
Nachoshangaa kila mtu anawapigia kelele TRA lakini hawaachi, kuanzia bosi mwenyewe, mawaziri wake, wabunge, mpaka sasa mkuu wa mkoa, lakini bado TRA hawana habari wanadunda zao tu..

Naamini inawezekana haya matamko ya kuwaonya TRA huwa ya kisiasa tu, wakienda kona wanaambiwa kazeni hapo hapo.
 
Haa haa tatizo mkuu wa nchi amepanic reli bado haijasha , stigla, bado watumishi wanamdai mishahara.yeye huwa anawajali zaidi wamachinga Kule yule anayelipa kodi ya 3m kwa mwaka
 
Nachoshangaa kila mtu anawapigia kelele TRA lakini hawaachi, kuanzia bosi mwenyewe, mawaziri wake, wabunge, mpaka sasa mkuu wa mkoa, lakini bado TRA hawana habari wanadunda zao tu..

Naamini inawezekana haya matamko ya kuwaonya TRA huwa ya kisiasa tu, wakienda kona wanaambiwa kazeni hapo hapo.
Hahahaaaa......!

Zilongwa mbali zitendwa mbali?
 
Back
Top Bottom