RC Mbeya aagiza Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kukamatwa na Polisi kufuatia kikao chake na Machinga

Siasa za kibabe. Haingii akilini kila mtu aviunge mkono vitambulisho vya kununua. Wagawe bure kama nia ni kuwatumambua. Mbunge wa upinzAni walitaka avisifie??
 
Hivi huwa mnacomment kwa kutumia busara ipi?
Kama Sugu hakufuata sheria achukuliwe hatua , ila mkuu wa mkoa kama kosa liko kwake apuuzwe. Sheria zimetungwa kunyanyasa wapinzani au wenye mawazo mbadala tu? Umenichefua na kuniharibia asubuhi yangu nzuri.
Hapa naliona kosa lake ni Uchochezi na sii Mkutano huo kwa sababu tozo ya Tsh 20,000 kwa wauza mbogamboga ni tozo za Halmashauri yaani Serikali ya mitaa, sasa anaposema atalipeleka swala hilo Bungeni nashindwa hata kumuelewa Sugu alimaanisha nini zaidi ya kuchochea Wananchi wadhani tozo hizo ni za Serikali Kuu na hivyo kuuchukia Uongozi wa Magufuli.
 
Wewe mtoto wa kiume acha kupenda vitu vya bure machinga tunajuana sisi tunaofanya hizi kazi za kimachinga kwa taarifa yako kwa machinga anae jielewa hawezi shindwa kulipia kiasi hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini alipe? kitambulisho kinamsaidia nini, hatolipa kodi? au ndio kitaleta wateja? Huku juu wanasema wanawasaidia machinga, wakati wao ndio wanajisaidia, manchapisha vitambulisho havina picha wala jina la muhusika,na aina ya biashara nayayofanya. Kitambulisho gani hicho sasa, si uhuni huu. Mimi nikikinunua leo nakitumia kesho Nampa jirani yangu utajuaje ni chake au sio chake? na kwanza kinafaida gani kwa mmachina? Mgesema ukweli serikali inatafuta pesa.
 
Vipi RC anasema nini kuhusu ajari za mbeya mbona hazipungui yeye anangoja nini kujiuzuru????
Mkuu wa MKOA WA MBEYA(ameagiza MBUNGE wa Mbeya MJINI Ndg. JOSEPH MBILINYI( RAIS wa Mbeya) AKAMATWE na POLISI kufuatia kikao chake na wafanyabiashara ndogox2 waliokuwa wakitoa KILIO kwa Mbunge wao kufuatia KULAZIMISHWA kununua 'VITAMBULISHO' vya Machinga'



======

Kamanda wa Polisi Ulrich Matei amethibitisha kumuhoji Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kwa kukashfu vitambulisho vya Serikali

Imeelezwa kuwa Mbunge huyo ameonekana kulikosoa zoezi la kugawa vitambulisho kwa Wafanyabiashara wadogo kwa kutumia kauli za uchochezi

Kamanda Mtei amesema kauli za Mbunge huyo zilijaa kashfa na kebehi

======
Updates:

SUGU ANYIMWA DHAMANA, KULALA RUMANDE

Mbunge huyo wa Jimbo la Mbeya Mjini aliitwa kuhojiwa na RPC wa Mkoa huo kwa tuhuma za kutoa kauli ya uchochezi

Mbunge huyo anatuhumiwa kwa kutoa kauli ya kuvikashfu vitambulisho vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya Wafanyabiashara


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnakosea, sheria haisemi uombe "kibali" bali "utoe taarifa 48hrs"kwa OCD wa eneo husika kabla ya mkutano....

Wanao kosea mkuu ni hao wapewa taarifa, wao wamegeuza sio kupewa taarifa bali ni kuombwa kibali. Unachezea policcm mkuu.
 
Kweli kabisa, tatizo chama cha kihuni mambo yao yanaenda kihunihuni tu, kama kavunja sheria asukumwe ndani tu. Kitambulishe atoe raisi pamoja na utaratibu wake yeye anadandia kvp
siutengeze chama chako mkuu kaa unaona chadema ni chama cha wahuni
 
Umeme mnataka, barabara mnataka, maji mnataka, madawa mnataka.

Kulipa kodi hamtaki, kodi haiombwi ni wajibu kila mtanzania alipe kodi kukingana na kipato chake.

Hatuwezi kupata huduma bora bila kuzigharamia kwa kodi zetu.
Kama nia ya Rais ni kuwasaidia wamachinga, kwanini visigawiwe bure hivi vitambulisho?! Msaada gani unanunuliwa?! Ukiondoa wenye kazi serikalini waliobaki wote machinga.
Kwani mbona walikuwa wanafanya vizuri tu hata bila vitambulisho?!
Kama uchumi uko tight, unadhani tungeambwa kuchangia kwa hiari mbona wangepata pesa nyingi zaidi ya hizi wanazopata kwenye vitambulisho?!

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni sawa na kumpiga teke chura.

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Back
Top Bottom