Nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba mkuu wa mkoa wa Mara kachanga 20m kwenye harambee ya Ccm kukusanya fedha kwa ajili jengo la CCM mkoa wa mara. Hii siyo haki kwani naamini fedha hizo hajazitoa mfukoni mwake bali bajeti aliyotengewa na Tamisemi/wizara ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya maendeleo ya wananchi. Ni vema akaeleza katoa fedha hizo kasma ipi? Na je atatoa fedha endapo chadema,TLP, CUF, NCCR n.k wakitaka kujenga ofisi zao za chama.Asipozitoa itakuwa ni ubaguzi wa kisiasa na nitaandika tena kumtaka azirejeshe 20m kwani zingeweza kujenga madarasa 3 ya secondary za kata au nyumba 3 za walimu au wafanyakazi wa vituo vya afya maeneo ya vijijini. Ikumbukwe hii ni fedha za walipa kodi watanzania.
Suala hili ni vema tukalikemea la sivyo litaota mizizi.Ukienda kwenye halmashauri za wilaya ndo utashangaa mwezi januari/februari nilikuwa tabora.Nilipata taarifa toka kwa watendaji wa wilaya kuwa magari ya CCM yanapata petrol/diesel toka depot na fungu la bajeti la wilaya, na hawalipii mafuta hayo matokeo yake fedha ya bajeti iliyotengwa inaisha mapema na kuwalazimisha maafisa kupunguza kazi za kwenda kusimamia masuala mbalimbali katika kata na vijiji. Je kweli hii ni haki ccm inayopata ruzuku kubwa toka serikali kupata mafuta ya bure toka serikali ya wilaya.Mbona vya upinzani havipewi mafuta hayo.Mbaya zaidi magari ya serikali yanafanya kazi za kichama CCM.
Ni vema tulione suala hili kama ufisadi/wizi na tulipigie kelele ili mkuu wa mkoa mwingine asichote 20m kupeleka kujenga jengo au shughuli ya ccm.Tulikemee ili mafuta wanayopata ccm bure wilayani yatumike kujaza mafuta magari ya ambulance ili yabebe wagonjwa hasa kina mama wajawazito na watoto wadogo wanaokufa kila kukicha kwa kukosa huduma muhimu za afya kwa sababu wapo mbali na zahanati na hospitali.
Mungu ibariki Tz ili tukate mizizi na mirija ya ufisisadi katika ngazi zote za utawala.
Nawasilisha kwa mjadala