RC Mara anaibua upya mgogoro wa Nyamongo

Jul 23, 2018
34
125
MKUU WA MKOA WA MARA ANAVUNJA SHERIA HII KWA MAAGIZO YA NANI?

Utulivu wa wakazi wa Mji wa Nyamongo Wilayani Tarime uliodumu kwa takribani miaka mitano sasa, unaanza kuvurugwa tena na Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndg. Adam Malima.
(Tafadhali soma mpaka mwisho)

Mwaka 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho ya sheria ya madini kwa kuzingatia vilio vya Wananchi wanaokaa maeneo ambayo madini mbalimbali huchimbwa.
Katika marekebisho ya sheria hiyo, Sheria inamtaka mwekezaji binfasi au kampuni inayowekeza katika uchimbaji wa madini ihusike katika kufanya maendeleo kwa Wakazi wa eneo lilalozunguka mgodi chini ya kitu kinachoitwa "Corporate Social Responsibility"
Lakini sheria hiyo pamoja na mambo mengine, inaelekeza kwamba, mwekezaji atakaa na serikali ya mtaa au kijiji husika ili kupanga miradi ya maendeleo kulingana na vipaumbele vya eneo husika.

Kwa kunukuu sheria hiyo ya Miscellaneous Amendment No.7 of 2017 katika kifungu cha 105 kinasema;

105.-(1) A mineral right holder shall on annual basis,prepare a credible corporate social responsibility plan jointly agreed by the relevant local government authority or local government authorities and the Minister responsible for local government authorities and Minister responsible for Finance.

Katika kipengele cha tano, sheria inatoa tafsiri zaidi juu ya "eneo mahususi".

(5) In this section " host communities " means inhabitants of the local area in which the mining operations activities take place.
Kwa tafsiri isiyokuwa rasmi ni kwamba;
"Katika kifungu hiki,host communities itamaanisha, wakazi wa mtaa au kijiji husika ambapo shughuli za uchimbaji madini zinafanyika".
Hivyo basi kwa tafsiri hii, ni sahihi kusema kuwa, pesa zinazotolewa chini ya CSR hazipaswi kwenda nje ya Kata/Kijiji chenye mradi huo.

Sasa Sheria imevunjwa wapi?

Ni takribani wiki tatu sasa, tangu RC Adam Malima atangaze kuchukua fedha za Mgodi wa Nyamongo za mfuko wa Corporate social responsibility kuzitoa kwenye eneo husika la mgodi (kama sheria inavyoelekeza) na kuzipeleka Mkoani.
Kiasi cha takribani TZS Bil.5.3 zimechukuliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (kinyume na sheria) na kuwekwa kwenye akaunti ya Mkoa.

RC huyo sasa amegeuka kuwa PAY MASTER GENERAL wa Mkoa, yeye ndiye Halmashauri na kila idara.
Kwamba leo hii fedha za Mgodi wa Nyamongo zinatolewa kwa wakazi wa Nyamongo wanaopata madhara ya moja kwa moja kutolokana na mgodi huu kisha zinapelekwa Wilaya zingine ambazo kimsingi hazipati madhara ya mgodi huu.

Ifahamike wazi kuwa, mwekezaji wa mgodi analipa kodi ya kisheria kwa sheria, maana yake Mgodi haudaiwi fedha za kodi. Lakini Serikali hii ya Rais Magufuli imeona kodi hiyo haitoshi sasa imeamua kuwapora wananchi fedha zao za halali. Huu ni wizi wa wazi, na hautakiwi kufumbiwa macho.
Kama RC huyu ametumwa na Boss wake ambae ni Rais Magufuli kufanya hivyo, basi Rais ajue kuwa wananchi wanalia na kulalamika sana kwa kitendo hiki kilichofanywa na RC.

Halmashauri ya Tarime Vijijini ni mwaka wa tatu sasa haijapokea fedha za serikali kutoka Serikali kuu, lakini miradi mbalimbali imekuwa ikitekelezwa kwa kutumia fedha za makusanyo ya ndani, ikiwemo pesa hii ya Mgodi.
Lakini sasa Halmashauri imeachwa ikiwa tupu, miradi iliyopangwa kujengwa kwa fedha hizi imesimama kwasababu tu imechukuliwa na RC kisha kuzisambaza Wilaya nyingine.

Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe. John Heche ni imani yangu kuwa taarifa hii tayari unaifahamu, tafadhali sana wasaidie kuwasemea Wananchi wako wa Nyamongo wanaolala na kuamka kwa milio ya baruti za migodi na kutumia maji yenye kemikali kutoka mgodini.

Siasa hii anayoifanya RC Malima, ni siasa mbaya sana, ni siasa inayoacha madhara makubwa kwa Wananchi,kuwakosesha huduma za maendeleo.
Watu wa Nyamongo wanasema hawapo tayari kuacha fedha zao ziende kiholela!!
Hawapo tayari!! Na hilo wamelisema wazi na wanaendelea kulisema.
Uvunjifu huu wa Sheria za nchi katika awamu hii ya tano umekuwa jambo la kawaida sana.

Nashauri Jambo hili RC aachane nalo,awarudishie Wananchi wa Nyamongo fedha zao.
Hatupendi kurudi kule Nyamongo ilikotoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,700
2,000
Kwanza kashamaliza kuuza vitambulisho vya wamachinga!?
IMG_20190223_200205.jpg
:):):)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom