RC Makongolo wa Rukwa, Ashitukia Upigaji wa pesa za Umma Milioni 570 Kwa Kujenga Majengo 2 Badala ya 5 ya Kituo Cha Afya Kate

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
47,634
55,571
Yaani Nchi nzima Serikali imekuwa ikitoa Milioni 570 za kujengea Majengo 5 yanayotosha Kuanzisha Kituo Cha Afya ila huko Rukwa Wajanja wamezitafuna.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi RC Makongoro Nyerere ameagiza uchunguzi uganyike na watu kuchukuliwa hatua Kwa kutafuna pesa zote Milioni 570 zilizotolewa na Serikali Kwa Ajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Kate Wilayani Nkasi huku Wakijenga majengo 2 tuu badala ya 5 na pesa zimemalizika.

Swali la kujiuliza ni kwamba yote hayo yanafanyika DC ,DSO,Kamanda wa Takukuru Wilaya yupo na Viongozi wengine walikuwa wapi wakati haya yakiendelea Hadi aje RC ndio ashituke na pesa zote zimeliwa?


My Take
Hii Nchi ni ngumu sana.
 
Waafrika hujirudisha wenyewe nyuma kwa tamaa ya fedha na kukosa uaminifu.Ni aibu sana watu wateseke kupata huduma huku watu walipewa wakaamua kugawana.
Bila Wananchi kuliamsha hakuna kitakachobadilika.
 
Back
Top Bottom