RC Makonda yuko Clouds FM, akanusha kutoa kauli ya kuwasaka wasio na kazi maalum nyumba kwa nyumba

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
952
346
Amesema yeye lake in chini ya Ulinzi na usalama. Aliwaagiza wenyeviti wa mitaa kufanya utambuzi wa watu katika mitaa yao. Najiuliza hivi wenyeviti huwa hawawajui wapiga kura wao?
13709769_1143831608993589_4802138192572607570_n.jpg

"Taarifa zilizoenea za kuwakamata vijana wasiokuwa na kazi zimechukuliwa katika namna ambayo sivyo nilivyoteuliwa na Rais wangu Dkt John Magufuli nilifanya mkutano na Wenyeviti wa Mitaa ambao wana mamlaka makubwa sana kwenye mitaa yetu na katika mambo mengi nilioongea nao nilizungumzia suala la ulinzi na usalama wa maeneo yetu nikatoa maelekezo mambo mawili, kwanza wawatake wananchi wao wafahamike kwenye serikali ya mtaa na pili wajue shughuli wanazofanya wananchi wao, mambo haya yanajenga misingi ya usalama na amani katika mitaa yetu, kuwafahamu wananchi wanakupa nafasi shughuli wanazofanya na ukijua shughuli wanazofanya kunakupa nafasi uko salama kiasi gani katika mtaa wako"

"Sijasema wasio na kazi wakamatwe na je ukiwakamata utawaweka kwenye magereza ipi? Lipo kosa la uzururaji una taratibu zake wapo watu nafahamu wapo watu hawataki tu kufanya shughuli na ndio hao hao wanakesha kwenye mitandao ya kijamii wamejipa hiyo kazi kama ajira, hivi unaona raha gani kila siku kutumia 'Instagram' na unamuona alianzisha mtandao huo kila siku anabuni na kuongeza uwezo wa matumizi ya 'instagram' halafu wewe unachekelea kutumia 'instagram' kwa ajili ya vitu visivyofaa, kazi yao ni kubuni magroup ya 'wathsaap', kutengeneza akaunti feki za majina ya viongozi"

Nimeongea na Waziri Mkuu kuona jinsi tunaweza kufanikisha Walimu kupanda mabasi ya mwendo kasi bure. Nia ya Rais Magufuli JP watoto kusoma bure lazima ikamilike. Ndio maana tunapigana kuwaondoa omba omba

Ikiwa ni siku chache imesemekana kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, amenukuliwa kuwa atafanya msako wa watu wasio na kazi maalum nyumba kwa nyumba, sasa anasema HAJAWAHI KUSEMA HIVYO na amadai watu wamemwelewa kinyume.

Asema kuwachukulia Hatua za KINIDHAMU waliotunga kuhusu Tamko la MEYA WA JIJI kuwa amebatilisha tamko la Mkuu wa mkoa (adai pia huo ni uongo meya hajasema chochote)

Chanzo: CLOUDS Redio Power BreakFast. (18/07/016)
 
Ikiwa ni siku chache imesemekana kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, amenukuliwa kuwa atafanya msako wa watu wasio na kazi maalum nyumba kwa nyumba, sasa anasema HAJAWAHI KUSEMA HIVYO na amadai watu wamemwelewa kinyume.

Asema kuwachukulia Hatua za KNIDHAMU waliotunga kuhusu Tamko la MEYA WA JIJI kuwa amebatilisha tamko la Mkuu wa mkoa (adai pia huo ni uongo meya hajasema chochote)



Chanzo: CLOUDS Redio Power BreakFast. (18/07/016)
 
Amesema yy lake in chini ya Ulinzi na usalama. Aliwaagiza wenyeviti wa mitaa kufanya utambuzi wa watu ktk mitaa yao. Najiuliza hivi wenyeviti huwa hawawajui wapiga kura wao?

Kwani tokea Uchaguzi upite hadi leo zimepita siku ngapi? Hivi haiwezekani kuwa tokea Uchaguzi umalizike mpaka leo hii tukawa tuna Wageni wengi wale wa halali na wasio halali waliopo nchini? Hivi kwanini Watu hatujui KUFIKIRI na tunachokijua kila mara tu ni kutanguliza CHUKI na SIASA mbele ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda? Huwa sipendi ninapoamka asubuhi halafu niki log in tu JF nakutaka na " UPUUZI " wa aina hii kutoka kwa Mtu ambaye eti nae anajiita GREAT THINKER. Sijui ni lini Watu wasio na AKILI watapungua AFRIKA!

Mheshimiwa Mkuu wangu wa Mkoa Paul Makonda piga KAZI " Kijana " na utunyooshe wana Dar es Salaam kwani wenye UPEO mkubwa tunajua kuwa unayoyafanya hayana tu maslahi kwa Wana CCM bali ni kwa Wana Dar es Salaam wote hata wakiwemo wa Vyama vingine na tutakupa kila aina ya USHIRIKIANO ili ufanye kazi yako vizuri kwani tuna IMANI na Wewe na haya MAJUNGU yafungie " vioo ". Tumechoka sasa kwani hakuna ambalo Makonda atalifanya hata kama ni JEMA kwetu lazima tu " mijitu " italeta politics.
 
Back
Top Bottom