streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 475
Inazidi kuleta matumaini kwa watanzania kwa kitendo cha mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda kujitwisha mzigo wa kutokomeza madawa ya kulevya yanayoathiri taifa letu hasa vijana. Harakati zake kuanza na wasanii ni njia nzuri maana wao ndio kioo cha jamii. Lakini RC hasiishie to kwenye Unga ila atie miguu hadi kwenye matumizi ya pombe aina ya viroba, kwa sababu ukiondoa madawa ya kulevya viroba vinaongoza kudhorotesha, afya na akili ya vijana hata wazee mpaka kufikia kudhorotesha na uchumi wa taifa. Mifano tunayo mitaani jinsi vijana wanavyohusudu pombe hizi huku wakijirundika vijiweni bila kazi za msingi. Ni rai yangu kwa RC na viongozi wengine kulivalia njuga swala hili ili kutengeneza Tanzania Imara.