MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Juzi juzi hapa uliita watendaji wa serikali za mitaa mkoa wa DSM ukawa live kwenye media takribani masaa 4 ukiwa umesimama ukiongea! Jumamosi nasikia umewaalika Wananchi kwa lile unachodai kusikiliza kero zao lakini utakua live tena kwenye vyombo vya habari, sasa kwenye media muda wote rafiki yangu kwanini usipige kazi kimya kimya kama wengine? Masaa manne umesimama live unaongea utafikiri Rais akilihutubia taifa! Haya utafika lakini tunakuombea.
Wapo wakuu wa mikoa waliowahi kuliongoza jiji la DSM kwa weledi mkubwa kimya kimya bila kutafuta coverage kwenye media na mpaka leo wameandika historia na majina yao hayawezi kufutika katika vinywa vya wakaji wa jiji hilo.Kazi ya kwenye media kila mara ni ya kufanya siasa na sio utendaji, Tenda kwanza media zitakufuata zenyewe na sio wewe kuzifuata.