RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kuna watu walikuwa wanakwenda nje ya nchi lakini hakuna kitu ambacho wamejifunza na Taifa likapata maendeleo.
Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya posta mlangoni,amesena kuwa teknolojia ya huduma hiyo watu walikuwa wanaona nchi nyingine lakini walishindwa kuleta nchini kwa maendeleo ya taifa katika huduma ya mawasiliano.
Amesema kuwa anamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kufuta safari za nje kutokana na kutokuwa na faida kwa watanzania huku akihoji kuwa waliokuwa wanakwenda walikuwa wanajiangalia wenyewe pamoja na familia zao na sio kuangalia taifa kwa masilahi mapana.
“Haiwezekani kwamba watu walikuwa wanakwenda nje ya nchi na wanaona jinsi ya huduma ya posta inavyofanya kazi kwa kupeleka vifurushi mlangoni kutokana na upangaji wa uwekaji majina pamoja na namba za kata lakini walishindwa kuchukua Teknolojia hiyo ni bora Rais Magufuli kafuta safari za nje”amesema Makonda.
Amesema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa huduma kwa wananchi atawaagiza wenyeviti wa serikali za mtaa kufanya mikutano na kuchagua majina ya mitaa yao.
Makonda amesema kuwa mitaa katika jiji la Dar es Salaam iko 573 hivyo huduma hiyo inatakiwa kuwafikia wananchi wa Dar es Salaam na kuacha kufanya safari zisizo na ulazima wa kwenda katika ofisi za posta.
Nae Kaimu Posta Masta Mkuu, Fortunatus Kapinga amesema huduma hiyo itakwenda kwa kasi kutokana na walivyojipanga na kodi za mitaa katika 32 wamefikia.