RC Makonda, nakuletea ombi na Jinsi ya kushughulikia kero za Wanafunzi wa jiji la Dar

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,382
7,817
MH: MAKONDA kwanza napenda nikupongeze kwa kupewa nafasi hii ya kuliongoza jiji letu la DSM! haikuwa ni bahati yako ila ni kwa kaz nzuri inayounganika na ubunifu ulionao katika kutatua kero mbalimbali! mungu akupe maisha marefu uweke historia ya kipekee kama kijana mwenzetu unayeonyesha njia katika uongozi!

Mh: mkuu wa mkoa leo nakuletea ombi la kushughulikia kero za wanafunzi wa jiji la DAR.

kama unavyojua mfumo wa usafiri kwa jiji ambavyo ulivyo, wamiliki wa vyombo vya usafiri ni watu binafsi, inakuwa taabu sana watoto wetu hasa wa shule za msingi kupata usafiri kwa wakati mfano asubuh kuanzia saa 12 mpaka saa 2 ni shda! makondakta ni wakali hawakubali kupakia watoto, mbaya zaidi na watu wazma ambao ni wazazi pia wanashuhudia usumbufu huo na wanapuuzia tu!

Mh: mkuu wa mkoa naomba kutoa mapendekezo ya namna ya kupunguza tatizo hlo na ninaamini itawezekana kwa uwezo wako kama ulivyoweza kwa WALIMU kusafiri bure!

1. Naomba ufanyike utafiti au upembuzi wa makini kubaini vituo ambavyo watoto wa shule husafiri kwa wingi halafu wawekwe askari POLISI kusimamia zoezi la kupakia watoto wa shule! ikiwezekana iwekwe idadi kamili ya kupakia watoto wa shule kwa kila daladala na POLISI awepo kuhakikisha hlo!

napendekeza polisi wakae asubuh kuwapakia kwenda shule na jioni kuwarudisha watoto.

2. suala la kuchajiwa 200 kwa watoto wa shule LIENDELEE tu hvohvo kwa kuwa ukisema iwe bure kama walimu itazua mjadala mkali itakuwa ni vurugu!

3. Nauli hii ya 200 iwe ni kwa njia zote mpaka njia za UDART ili kuleta usawa! mambo ya kuweka nusu ya mtu mzima YAFIE MBALI kwani itajenga matabaka miongon mwa watoto maskin ambao ndo wengi!

hawa UDART walipendekeza naul ya mwanafunzi iwe nusu, mfano kama kutoka MBEZI--KIVUKONI ni 1200/ mwanafunz atalazimika kulipa 600, hili LIKATAE kwa nguvu zako zote! nauli ni 200 tu jijini kwa watoto wa shule! usiruhusu UDART watuvurugie mfumo wa maisha na kutufanya tuwaze mambo ya kifisadi!

4. Kupata wasomi bora kwa taifa letu kunaanzia na kupunguza kero hizi za usafiri, ukichunguza vizuri utakuta viongozi wengi wa tanzania wametokea familia maskini lakin wakishapata maisha wanatembelea magari ya kifahari wanasahau kuwa kuna kujenga taifa la kesho!

ni hayo tu mh: makonda

nakusalimu kwa jina la maendeleo na hapa kazi tu.
 
nashukuru ma mods kwa kunirekebishia heading ili ieleweke vizuri! asante
Kuwa na mfumo unaojiendesha na kujisimamia wenyewe ndio njia nzuri ya kutatua matatizo. Haya mambo ya kusimamia usafiri wa wanafunzi kwa polisi (ambao ni haba) ni mpango wa kizamani sana. Siungi mkono kabisa wazo lako. Njia nzuri ya kupambana na tatizo la usafiri Dar, kwa wanafunzi , ni kuwa na barabara zinazokidhi mahitaji na vyombo vya usafiri vyenye uwezo wa kubeba abiria wengi eg train, tram and metro. Halafu serikali inatakiwa i-subsidize pengo la nauli pungufu wanayolipa wanafunzi. Nina uhakika fedha zipo kama mipangilio itakuwa mizuri na ufisadi na ubaridhifu wa mali ya umma utapigwa vita. Hakuna shortcut ya mafanikio kama wengi tunavyotaka.
 
Ndugu yangu iamini tu serikal ya magufuli tutafika tu huko unakokutamani! kwa sasa tushughulikie kero iliyopo mbele yetu!
 
Back
Top Bottom