RC Makonda na Mambosasa, kwa hili la baadhi ya watu kutokuvaa barakoa DSM mnamuangusha Rais

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,872
Wakuu amani iwe kwenu,

Rais Magufuli mara nyingi amesisitiza watu kuvaa barakoa ili kujilinda na kulinda wenzao dhidi ya kuenea kwa ugonjwa hatari wa corona. Rais amesisitiza sana hili na nilitegemea viongozi wa chini akiwemo Mkuu wa Mkoa DSM, Wakuu wa wilaya zote, Kamanda wa kanda maluum ya DSM na Wakuu wa polisi wa Mikoa ya kipolisi zote za DSM wamsaidie mheshimiwa rais kuhakikisha agizo hilo la watu kuvaa barakoa linatelekezwa vyema ila wapi.

Leo ukipanda daladala ya kwenda popote DSM utakutana na watu wachache sana wamevaa barakoa inavyopaswa, wengine wanavyo wamevaa ila kaacha pua nje, mwingine anayo ila kaishusha chini ya kidevu, mwingine anayo ila kaiweka kwenye paji la uso, mwingine kaishikilia mkononi tu na wengi hawana kabisa.

Sasa kama mheshimiwa Rais kasema watu wavae barakoa halafu wanakaidi kuvaa huku wakijua wanaweza kueneza au kupata kwa kutokuvaa halafu nyie viongozi wa chini nao mko kimya mnategemea nini?. Ina maana RC Makonda na kamanda Mambosasa hamjui kwamba watu wanakaidi hii amri halali kiafya tena ombi la mheshimiwa rais ambalo ni amri kabisa kama mnavyotuamisha kila siku?

Hivi kwanini viongozi wetu mnapenda kiki tu kwenye mambo ya kisiasa badala ya haya mambo ya muhimu? Juzi kuna vijana wa CHADEMA wamekamatwa huko sijui Iringa kwa kugawa barako badala ya polisi kushughulika na wasiovaa barakoa. Hivi ni lini Mheshimiwa rais kakataza chama, au raia kuchangia barakoa au ndoo za maji? Kama ipo mimi sijasikia ila nimesikia akisema watu wavae barakoa. Sasa wa kumkamata ni nani? Anayegawa barakoa kukinga watu au anayekaidi kuvaa tena kitu cha sh 500 hadi 1000 na kibaya wakati mwingine anayo mkononi.

Rais alipotangaza kusitisha maandamano na mikutano ya hadhari mpaka 2020 kila RC na RPC aliitikia kwa nguvu zote hadi vikao vya ndani ambavyo hamkuambiwa kukataza lakini kwa hili la Corona mko baridi huku watu wakiendelea kuambukizana, mnataka Mheshimiwa Rais aseme kwamba kuvaa barakoa ni sheria na ambaye hatavaa atawajibishwa ndiyo muanze kazi?

Kama kila kitu mpaka muambiwe mnasubiri nini huko ofisini? Tena cha hatari ni kwamba traffic wetu hawajali kuhusu kondakta, dereva wala abiria asiye na barakoa (pongezi kwa traffic wachache wanaokumbusha watu). Kuhusu barakoa kusiwe ni utani iwe ni sheria na itekelezwe kwa hiari na shuruti kwa asiyetaka hasa kwa DSM.

Watu wa TEMESA pale Ferry mwanzoni mliweka vijana wa SUMA JKT kusimamia unawaji na kulazimisha watu wavae barako kabla ya kuvuka, upande wa barakoa naona mnajitahidi japo wengine bado wanakadi ila kuhusu kunawa kumeshakuwa kama hiari tu wengine hawanawi japo maji yapo kwasababu vijana wa suma hawasimamii tena.

Chondechonde Mkuu wa Mkoa na Ndg. Mambosasa, tusaidieni kuwashughulikia bila huruma wanaokaidi kuvaa barakoa, hii iwe sheria halali yenye adhabu kali. WHO wanasema huu ugonjwa lazima tujue namna ya kuishi nao sasa kama wakati huu walau mikusanyiko inakatazwa na shule zote zimefungwa watu hawavai barakoa wala kunawa pale tutakaposema jamani huu ni ugonjwa wa kudumu tuishi nao hivyo hivyo kama UKIMWI nani atavaa barakoa? nani atanawa? watu wataendelea kupiga chafya na kukohoa kama mbuzi .

Nasisi Watanzania sijui tukoje jamani kusimamiwa hadi kwenye vitu vya kawaida kama kuvaa barakoa, huko kwa wenzetu wanaoanza kuruhusu shughuli ziendelee wana akili , wanasikia na kufuata ushauri wa watalaamu ila huku kwetu ni changamoto tuna jamii za watu wajinga wasioelewa wala kutii mamlaka.

Nb: Suala la Corona ni la mtu binafsi kisha la familia halafu baadaye la taifa ukifa wewe hasara ni yako na familia yako chukua tatua kemea anayetaka kukuambukiza kwa kutokuvaa Barakoa.

Kindikwili.
 
Ww tu ndo hujaona mm jana nimeshuhudia watu wameshushwa na polisi kwenye daladala za masaki-kariakoo kisa hawana barakoa mkuu sijajua kwa route nyngne ila ukipta daraja la sarenda lzma mtapigwa search tu kama huna unashushwa ukinunua ndo unaendelea na safari zako.

yess BishOoo haSwaaaaaaaH
 
Ww tu ndo hujaona mm jana nimeshuhudia watu wameshushwa na polisi kwenye daladala za masaki-kariakoo kisa hawana barakoa mkuu sijajua kwa route nyngne ila ukipta daraja la sarenda lzma mtapigwa search tu kama huna unashushwa ukinunua ndo unaendelea na safari zako

yess BishOoo haSwaaaaaaaH
Mkuu hiyo route uliyotaja ndiko wanakoishi binadamu ujue, so ukaguzi lazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww tu ndo hujaona mm jana nimeshuhudia watu wameshushwa na polisi kwenye daladala za masaki-kariakoo kisa hawana barakoa mkuu sijajua kwa route nyngne ila ukipta daraja la sarenda lzma mtapigwa search tu kama huna unashushwa ukinunua ndo unaendelea na safari zako.

yess BishOoo haSwaaaaaaaH

Hao nimewapa kongole kwenye uzi BishOoo
 
Na huu mtindo wa trafiki kusimamisha dala dala halafu yeye hata haji kukagua GARI wala abiria. Anamsubiri konda amfuate huko nyuma kabisa alikosimama. Halafu konda akumfuata "wanafanya yao" halafu konda anarudi kwenye gari na safari inaendekea.

Sasa mtu unajiuliza, huyu trafiki alisimamisha gari ili "asalimiwe" tu na konda? Huko ndani ya gari kuna watu kibao hawana barakoa hata konda mwenyewe barakoa ilikuwa kidevuni na aliirekebisha ndo akamwendea trafiki.
Napendekeza:

1. Iwe ni marufuku kwa konda kuruhusu abiria asiyevaa barakoa kwenye gari na yeye mwenyewe awe amevaa barakoa muda wote
2. Trafiki wahakikishe wanasimamisha magari ya abiria/dakadala na kukagua wasiovaa barakoa.
3. Kama abiria kwenye gari hana barakoa, konda apigwe faini ya hapo hapo na abiria ashushwe kwenye gari, apigwe faini ya hapo hapo na pia achapwe viboko hapo hapo kama wanavyofanya India.

Hii ni vita na tusiwe na simile hata kidogo.
 
Ni rais yupi wanayemwangusha? Huyu huyu ambae aliongea hadharani kwamba tiba na kinga ya kweli ni imani kwa sababu barakoa ni matambaa tu ya puani, au?

Anyway, hao ambao hawavai barakoa wanajua wanachokifanya! Badala ya kutegemea mavitambaa ya puani, wao wameamua kutegemea imani kama alivyosema rais.
 
... umeeleza kitu muhimu sana Mkuu! Halafu kuna wengine akitaka kuongea na simu anavua barakoa (nadhani ili sauti itoke vizuri) na baadhi unakuta mtu anaonge safari nzima huku akimwaga mimate kwa abiria wengine.

Mwingine akitaka kupiga chafya au kukohoa anavua barakoa; anona kama inamzuia kutoa kikohozi au chafya vizuri kumbe ndio hivyo anamwaga makohozi kwa wengine! Inaonekana hii nchi ina wajinga wengi kuliko mahali pengine popote duniani.
 
Bila hivyo watu wataambukizana mpaka wote wawe na ugonjwa halafu inabaki ile survival of the fittest
Kuna wengine hawajali kabisa!! Watu wa namna hiyo ni wauaji na tusiwachekee!! Nikiona clip moja huko India polisi wanachapa viboko wote waliokuwa wanakiuka lockdown. Kama kuna mtu anayo hebu atuwekee hapa tena ili watu waone jinsi wenzetu walivyo serious!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... umeeleza kitu muhimu sana Mkuu! Halafu kuna wengine akitaka kuongea na simu anavua barakoa (nadhani ili sauti itoke vizuri) na baadhi unakuta mtu anaonge safari nzima huku akimwaga mimate kwa abiria wengine...
Makonda pia unakuta anatangaza vituo kwa sauti kubwa huku akipita anatoza nauli na anasambaza mimate yake wakati barakoa kaishusha kidevuni au kaiweka mfukoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanamwangushaje wkt rais mwenyewe havai hayo madude na wanadsm wengi wanayavaa kidevuni.
 
Wakuu amani iwe kwenu,

Rais Magufuli mara nyingi amesisitiza watu kuvaa barakoa ili kujilinda na kulinda wenzao dhidi ya kuenea kwa ugonjwa hatari wa corona. Rais amesisitiza sana hili na nilitegemea viongozi wa chini akiwemo Mkuu wa Mkoa DSM, Wakuu wa wilaya zote, Kamanda wa kanda maluum ya DSM na Wakuu wa polisi wa Mikoa ya kipolisi zote za DSM wamsaidie mheshimiwa rais kuhakikisha agizo hilo la watu kuvaa barakoa linatelekezwa vyema ila wapi...
Naamini kabisa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Dar utaguswa na hisia za wakazi wako na kero yao kuhusu ukiukwaji ya maelekezo ya serikali kuhusu kuepusha kusambaa kwa maambukizi ya corona kwenye usafiri wa umma. Tunakuamini utalishughulikia jambo hili ili watu tuwe na amani.
 
Na huu mtindo wa trafiki kusimamisha dala dala halafu yeye hata haji kukagua GARI wala abiria. Anamsubiri konda amfuate huko nyuma kabisa alikosimama. Halafu konda akumfuata "wanafanya yao" halafu konda anarudi kwenye gari na safari inaendekea...
Nafikiri hapo Dar watu wanacheza na corona itakapo changanya itakuwa kiama.
 
Back
Top Bottom