Paul Makonda: Lowassa angekuwa Rais ningekuwa jela muda huu

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
"Mimi nimemkataa Lowassa kipindi bado anatisha , mungemchagua ningekuwa jela muda huu

Mimi nilimkataa tokea Niko Umoja wa vijana namkumbuka niliitisha press na waandishi wa habari nilipotamka kwamba Lowassa hafai kuwa Rais mmoja alidondosha glass Kwa kuogopa, na waandishi wa habari wakakimbia kuniachia makamera mimi,

Hivo nilimkataa bado akiwa anatisha siyo mda huu hana nguvu tena"

Mwisho wa kumnukuu makonda
 
Hii ndio video ya Makonda alipomsema Lowassa ambapo ilipelekea mwandishi aangushe glasi!

Ninachojua Makonda hakwenda kama Makonda bali kulikuwa na kikundi cha watu kilimtuma. Ninampongeza kwa ujasili kwa sababu kuna wengine wasingefanya kutokana na nguvu aliyokuwa nayo Lowassa.

Sio uwongo, Lowassa wa wakati huo alikuwa moto ndani ya CCM na nje ya CCM!

Lowassa wa wakati huo ndio alifaa kuitwa ''kamanda'' na sio leo eti CHADEMA wanamuita kamanda wakati amekuwa kama nyoka asiyekuwa na sumu ya kisiasa.

kuna kampeni sahvi?hana shughuli yakufanya mpaka amuwaze luwasa?vp dady akitoka atakuwa salama kwa matendo yake?haoni mfano kwa sumaye kwa zaidi ya miaka kumi alikuwa pm leo anaburuzwa na wakuu wa wilaya?leo sumawe angeweka mazingira bora ya utawala yangemkuta ya leo?hv ni vyeo tu na vya mpito leo kwako kesho kwangu.
 
"Mimi nimemkataa Lowassa kipindi bado anatisha , mungemchagua ningekuwa jela muda huu

Mimi nilimkataa tokea Niko Umoja wa vijana namkumbuka niliitisha press na waandishi wa habari nilipotamka kwamba Lowassa hafai kuwa Rais mmoja alidondosha glass Kwa kuogopa, na waandishi wa habari wakakimbia kuniachia makamera mimi,

Hivo nilimkataa bado akiwa anatisha siyo mda huu hana nguvu tena"

Mwisho wa kumnukuu makonda

Nmejikuta nacheka tu
 
Yeye anajiona shujaa kwa kusema Lowassa hafai kuwa rais, wakati hajawahi kuwa rais, wakati huo huo kuna watu wanasema Magufuli hafai kuwa rais kwa kuwa ni dictator tena akiwa madarakani. Alitakiwa atokeze hadharani na kusema rais aliyeko madarakani hafai hapo ningemuona shujaa. Na kwa jinsi huyo dogo alivyo mnafiki leo hii Lowassa angekuwa rais ndio angekuwa kwenye kamati ya kunyonga watu ili wasimpinge Lowassa.
 
Kwa hili namuunga Mkono Paul Makonda!

Watu wote ndani ya CCM walikuwa wanazunguka mbuyu na Hata Nape Mwenyewe alikuwa anazunguka tu Mara mapacha watatu Mara Sijui Mtuhumiwa wa Ufisadi

Ni Paul Makonda akiwa kwenye Kamati ya Uhamishajinya UV CCM ndio alithubutu kumtaja Edward Lowassa kwa Jina lake kwa kumwita Fisadi

Kwa Lowassa wa 2007-2015 ilihitajika roho ya ujasiri sana kumtaja kwa Jina Tena ukiwa ndani ya CCM maana Hata Jk wakati huo alikuwa hawezi kufanya hivyo
 
Yeye anajiona shujaa kwa kusema Lowassa hafai kuwa rais, wakati hajawahi kuwa rais, wakati huo huo kuna watu wanasema Magufuli hafai kuwa rais kwa kuwa ni dictator tena akiwa madarakani. Alitakiwa atokeze hadharani na kusema rais aliyeko madarakani hafai hapo ningemuona shujaa. Na kwa jinsi huyo dogo alivyo mnafiki leo hii Lowassa angekuwa rais ndio angekuwa kwenye kamati ya kunyonga watu ili wasimpinge Lowassa.
Kamati ya kunyonga watu ili wasimpinge Lowassa, ,kweli wewe ni tindo mwenyewe haswa!
 
Back
Top Bottom