RC Makonda: Kuna "Biological weapons" tujihadhari. Asema hata pale ukumbini walipo, zinaweza kuwepo bila waliomo kujua

Kasema vizuri kuhusu biological weapons? Unahakika umesikiliza kwa makini au ndio zile huba tuu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sina huba na huyu mtu. Kiukweli kawaasa watanzania kuangalia wanaohimiza demokrasia kwa macho mawili....kuna mataifa ya magharibi yanatumia democrasia kutimiza malengo yao....pia kasema kuwa makini biological na chemical weapons ....hapa kasema "kutumika mikononi hasa hand shaking"...it applies to both sides.
 
nimecheka sana yaaani hata aliyoongea hayaendani na mkutano..eti anachukia neno demokrasia hata wanaohubili demokrasia kwao haipo,eti hata katiba mpya haina haja kwani na wao hawana katiba mpya yaaani huyu kijana atawaabisha sana kwenye mikutano ya aina hii asipewe nafasi ya kuongea
Kwa nini alikubali Posho ya ujumbe wa Bunge la katiba kama anaona haina haja. Arudishe kama anavyotakiwa kurudisha za TASAF
 
2316672_uvccm.jpg

Ndio maana wanamlinda katibu ili asivamiwe na Nzige waliorutubishwa
 
Bwana huyu mbona kaongea vizuri tu...asingegusia kipengele cha pili salamu zake zingekuwa murua sana.

Hata biological weapon kasema in general terms na kutumia neno "huenda".

Tusimhukumu sana.

..hakutakiwa azungumzie demokrasia na kuikandia.

..unaposema UNACHUKIA demokrasia unawatisha badala ya kuwavutia wawekezaji na wenye mitaji.

..pia amepiga madongo katiba. Sasa katiba ndiyo inayosimika sheria, na sheria ndiyo zinaweka taratibu na miongozi ya uwekezaji na namna ya kufanya biashara.

..Ukipiga madongo katiba unaonekana hutaki kufuata sheria, na wawekezaji hawapendi kuwekeza mitaji yao ktk eneo lisilokuwa na utaratibu za kisheria.

..kwa kweli waliomualika kuzungumza bila kumuandalia hotuba nao wanastahili lawama.
 
Mkuu, maswali ni mengi kuliko majibu.

Hiyo mbinu mpya ya utekaji na uuaji imeshaanza kutumika hapa Tanzania?

Kwamba WASIOJULIKANA SASA WANATUMIA KEMIKALI?

AKAMATWE, AHOJIWE NA AELEZE KAONA NA KUSIKIA WAPI?

HII NI ZAIDI YA UHUJUMU.

AKAE NDANI BILA DHAMANA MPAKA KIELEWEKE.
 
Nzige akiwa amechorwa kwenye jiwe 4000bc
View attachment 1367269

View attachment 1367271
Nzige akiwa amechorwa kwenye Kaburi la Tutmoses wa tatu miaka 4000kabla ya yesu


Sasa leo anakuja mjinga mmoja kuwaaminisha wanaCCM kuwa ati wametengenezwa ili kumpiga vita Magufuli
Heheheee!!!...bhagoosha? Acheni bhongo yenu
Hawa jamaa inabidi wasaidiwe. Haiwezekani shughuli ya Kimataifa kama hiyo inaendeshwa kama ya kitaifa.... Actually, more kama vile ya Kichama.
 
Hii ni aibu kwa Taifa, hivi kuna ulazima gani huyu kuwa mkuu wa mkoa. Kwanini asipelekwe kuwa askari wanyama pori huko TANAPA!!! Mkutano mkubwa kama ule kumpafursa ya kuongea mtu ambaye hata elimu yake haijulikani ni aibu hata kwa aliyemteua.
 
hata hivyo nikimlaum Bashite ntakuwa ninakosea

just imagine kama aliweza kumkwida yule mzee mstaafu tena Live mbele ya macho na aliekwidwa ni mtaalam wa sheria..!??

the guy is the devil's himself

nzige ndiye yeye na democracy ndiye wao,

nadhani kuna ujumbe wa siri anautoa bila kutarajia,hasa dhidi ya mahasimu wake

*nimeona wajumbe wa mkutano wanashangilia kwa nidhamu ya woga ;hata wanaonesha mdani mwao hawajui kwa nini wanashangilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa anatahadharisha kwamba kutokana na vita vya kiuchumi wenzetu wanatumia silaha kibao. Some of the weapons ni "democracy " ambayo hata wao hawako vizuri. Weapon ya pili "wanaweza" kutumia hata biological weapon kama virusi n.k. hajasema "tayari nchini kuna biological weapon kama mada inavyosomeka". Mkiambiwa kwamba UFIPA mlishaishiwa AGENDA mmebaki na kudandia MATUKIO mnakasirika. Endeleeni hivyo hivyo mtaona at the end of the election nini mtaambulia
Kuna relevancy?
Mbona kama unajisemesha mwenyewe tu?

Hii hoja haitakuwa imekamilika unless umeambatanisha na hoja hiyo kwa video ama sauti!!
Tiiyari video Imeshawekwa na wadau
 
Kauli yake ya "nzige kutengenezwa na kusambazwa" inawezekana kabisa. Tatizo la bwana yule ni kuropoka.

Nzige ni salaha nzuri sana kwa nchi maskini....unazalisha mayayai tu na kutegea kuyamwaga majira ya kipindi mazao yanaanza kukua.
Mkuu, nzige na madini wapi na wapi? Are we serious kwa mkutano adimu na wa kimataifa kama ule??
 
Back
Top Bottom