Jamani sijaona mtu mbunifu kama huyu Mkuu wa Mkoa, amekutana na balozi wa china moja ya mazungumzo yao ni uwezekano wa kampuni za china kuja kufanyakazi za kuzoa taka na kutengeneza madawati.
Hawa wachina balaa watachukua condom chakavu na kutengeneza mawigi, pembe na nyeti za ng'ombe watatengeneza viagra. Yale malundo ya taka za matenga watatengeneza mbolea na machungwa na mananasi yaliyooza watatengeneza pombe ya kiroba, Machupa ya maji ya uhai watatengeneza viti na madawati ya wanafunzi. Yaani hakitatupwa kitu.
====================

March 23 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alikutana na Balozi wa China nchini Tanzania na kujadiliana kuhusu namna ya kuinua uchumi kwa vijana wa Kitanzania na kusaidia elimu kwa wanafunzi.
‘Balozi wetu wa china amekuja kunitembelea katika ofisini yangu na kufahamu ninashughulika na nini kwahiyo tulizungumza vitu kadhaa ikiwemo changamoto mbalimbali ikiwemo ya wadogo zangu kukosa madawati Lakini pia nimemuelezea changamoto ya usafi kwamba mji wetu kwa sasa hivi upo kwenye kampeni ya usafiri’ – Paul Makonda
‘Ningependa kuona katika makampuni yaliyopo tupate hata baadhi ya makampuni kutoka kwao pia yanayoweza kufanya usafi huo kwa maana kuchukua uchafu unaoonekana na kutengeneza mbolea na kuzalisha umeme’ – Paul Makonda