RC Makonda, Kova, washiriki kuzinduliwa uongozi mpya wa baraza la vijana wa kiislaam bakwata

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1472974472542.jpg
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, amewataka vijana wa mkoa wa Dsm kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo katika jiji la Dar es salaam, huku akiwataka kulipa kipaumbele suala la ulinzi na usalama pamoja na kuepuka kutumiwa ili kuvuruga amani kwa maslahi ya watu wachache.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa uongozi mpya wa baraza la vijana wa kiislaam wa baraza kuu la waislamu mkoa wa Dsm bakwata, alisema mkoa una fursa nyingi za kiuchumi ambazo vijana wakijipanga vizuri, wanaweza kuibua miradi mbalimbali na kwamba Serikali ya mkoa iko tayari kuwasaidia.

"Kuna fedha zaidi ya shilingi bilioni 20 zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya mitaa ya jiji la Dar es salaam "alisema

Aidha Makonda amesema, kumekuwa na tabia ya kubeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano, lakini akawataka wananchi kutokatishwa tamaa na kuaahidi kuwa changamoto zote zilizopo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi zikiwemo za ulinzi na usalama.
1472976298371.jpg

Mufti wa Tanzania sheikh abubakar zubairy bin Ally amelitaka baraza hilo la vijana kuzingatia katiba pamoja na majukumu yao na kuwaasa kutokuwa na fikra za kufanya mapinduzi ya viongozi wa bakwata au wa misikiti huku Kamishna mstaafu wa kanda maalum ya Dsm, CP Suleimani Kova akiwashauri vijana kujikita katika mambo ya uzalishaji mali pamoja na kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Source: Channel Ten
 
Bado wana uchungu wa kuipoteza dar kwa ukawa sasa wamepiga hesabu ili waweze kupata kura kwa wingi ni kuwa karibu na waislamu ambao wengi wao wapo pwani na misikiti mingi kipindi cha uchaguzi walikuwa wana hamasisha kupiga kura kwa wapinzani lakini kasahau kuwa kilio kikubwa cha waislamu sio ofisi bali ni mahakama ya kazi ambayo JK alishindwa kuitekeleza ingawa waliaidi kipindi cha kampeni.
Ushauri kwa makonda kama nia ni kura za waislamu abariki tu mahakama ya kazi atapata kura zote.
 
Hii ndio bakwata tunayoitaka kafir anatajengea nyumba ya ibada anahutubia baraza la maulamaa, idd ana futurisha any way nasubiria muanze kula chair fire niwakimbie rasmi
 
Mbona kila Siku Makonda na BWAKWATA kuna nini hapa katikati?
Wanatafuta wafuasi
View attachment 393337Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, amewataka vijana wa mkoa wa Dsm kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo katika jiji la Dar es salaam, huku akiwataka kulipa kipaumbele suala la ulinzi na usalama pamoja na kuepuka kutumiwa ili kuvuruga amani kwa maslahi ya watu wachache.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa uongozi mpya wa baraza la vijana wa kiislaam wa baraza kuu la waislamu mkoa wa Dsm bakwata, alisema mkoa una fursa nyingi za kiuchumi ambazo vijana wakijipanga vizuri, wanaweza kuibua miradi mbalimbali na kwamba Serikali ya mkoa iko tayari kuwasaidia.

"Kuna fedha zaidi ya shilingi bilioni 20 zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya mitaa ya jiji la Dar es salaam "alisema

Aidha Makonda amesema, kumekuwa na tabia ya kubeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano, lakini akawataka wananchi kutokatishwa tamaa na kuaahidi kuwa changamoto zote zilizopo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi zikiwemo za ulinzi na usalama.View attachment 393360

Mufti wa Tanzania sheikh abubakar zubairy bin Ally amelitaka baraza hilo la vijana kuzingatia katiba pamoja na majukumu yao na kuwaasa kutokuwa na fikra za kufanya mapinduzi ya viongozi wa bakwata au wa misikiti huku Kamishna mstaafu wa kanda maalum ya Dsm, CP Suleimani Kova akiwashauri vijana kujikita katika mambo ya uzalishaji mali pamoja na kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Source: Channel Ten
 
Bado wana uchungu wa kuipoteza dar kwa ukawa sasa wamepiga hesabu ili waweze kupata kura kwa wingi ni kuwa karibu na waislamu ambao wengi wao wapo pwani na misikiti mingi kipindi cha uchaguzi walikuwa wana hamasisha kupiga kura kwa wapinzani lakini kasahau kuwa kilio kikubwa cha waislamu sio ofisi bali ni mahakama ya kazi ambayo JK alishindwa kuitekeleza ingawa waliaidi kipindi cha kampeni.
Ushauri kwa makonda kama nia ni kura za waislamu abariki tu mahakama ya kazi atapata kura zote.
nafikiri ulitaka uandike Kadhi
 
Back
Top Bottom