RC Makonda: Jiji la Dar es Salaam liko salama, wananchi msiwe na hofu

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
158
500
Baada ya Tahadhari ya Usalama katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Masaki na Msasani iliyotolewa na Ubalozini wa Marekani, Mkuu wa mkoa wa Dar amewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari

RC Makonda amesema Jeshi la Polisi linaendelea na kazi kama kawaida kuhakikisha watu wanalala salama na walio kwenye mahoteli wasiwe na hofu ya tishio lolote lile

Aidha, ameomba watoa taarifa kuzigatia sheria, Kanuni na Katiba ya nchi kwani kuna vyombo maalumu vilivyopewa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
7,291
2,000
Hawa jamaa sijui vipi? Kwa hiyo mlikuwa mnataka wakae kimya tu wakati intelejensia yao imeonyesha kuna uwezekano wa kushambuliwa?

Yaani badala ya kushukuru mnalaumu. Si ajabu mngepewa hizi taarifa mngezikalia badala ya kuutahadharisha umma, wameona bora wao wautangazie uma kuepusha madhara.

Kuna ubaya gani katika hilo?. Badala ya kukanusha fanyieni kazi hizo rumours.

Wamarekani hawana sababu yoyote ya kutoa taarifa za uzushi.
We are always REACTIVE not PROACTIVE,

Unapewa info fanyia kazi sio kujifanya mjuaji
 

vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,091
2,000
... ni njia tu ya kuficha aibu baada ya intelijensia ya nchi ya kigeni kujua yajayo ndani ya nchi yetu wakati vyombo vyetu vimelala fofofo! Hakuna lolote hao; CIA ndio imewaamsha usingizini wanajifanya kujua kabla!
Kama Sirro na wenzie walishajua mapema kwa nini hawakutoa alert yao mapema kwa jamii lengwa?...ni muhimu kuweka siasa pembeni kwenye vitu vya hatari
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,312
2,000
Acheni dharau, mumeonan Mhe Msukuma bungeni anatoa material nzuri mpaka Rais kafukuzwa waziri wa viwanda na CEO wa TRA kazi? Wenye shahada na PhD niwaoga kusema ukweli, wanalindana!! Hongera Mhe Mkukuma(Mhe Joseph Kasheku)!
wakolomije bana, utawajua tu!
 
Top Bottom