RC Makonda: Jiji la Dar es Salaam liko salama, wananchi msiwe na hofu

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Baada ya Tahadhari ya Usalama katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Masaki na Msasani iliyotolewa na Ubalozini wa Marekani, Mkuu wa mkoa wa Dar amewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari

RC Makonda amesema Jeshi la Polisi linaendelea na kazi kama kawaida kuhakikisha watu wanalala salama na walio kwenye mahoteli wasiwe na hofu ya tishio lolote lile

Aidha, ameomba watoa taarifa kuzigatia sheria, Kanuni na Katiba ya nchi kwani kuna vyombo maalumu vilivyopewa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari
 
Hawa jamaa sijui vipi? Kwa hiyo mlikuwa mnataka wakae kimya tu wakati intelejensia yao imeonyesha kuna uwezekano wa kushambuliwa?

Yaani badala ya kushukuru mnalaumu. Si ajabu mngepewa hizi taarifa mngezikalia badala ya kuutahadharisha umma, wameona bora wao wautangazie uma kuepusha madhara.

Kuna ubaya gani katika hilo?. Badala ya kukanusha fanyieni kazi hizo rumours.

Wamarekani hawana sababu yoyote ya kutoa taarifa za uzushi.
 
Wenzenu ubalozi wa Marekani ni utaratibu wao kutoa alerts kwa raia wao waishio nchi husika kila siku kwenye website zao wanatoa update wala hawajaanza Leo wala Jana ni utaratibu wao. Sasa shida sisi tunafanya siasa tukijiaminisha Tipo salama?

Kwa level yetu tuposalama kwani Tz kupotea aukufa watu si kitu cha usalama regardless kimefanywa na Nani wao they are ready tu protect raia wao mmoja Kati Ya population Ya 330m kila mtu kwao ni muhimu
 
Sijaelewa lengo la Makonda ni nini kutaka tuzipuuzie taarifa za kiusalama.
At the end of the day kila mtu ataamua amsikilize Makonda na kujiachia kwenye mikusanyiko bila tahadhari au US Embassy kwa tahadhari.
Ningeweza ningeshauri watu wote waisikilize US Embassy kuliko Makonda. Mzaha mzaha tunaweza kulia kwa kusikiliza watu waliotaka watoe taarifa wao wa kwanza.
 
Hawa jamaa sijui vipi? Kwa hiyo mlikuwa mnataka wakae kimya tu wakati intelejensia yao imeonyesha kuna uwezekano wa kushambuliwa?

Yaani badala ya kushukuru mnalaumu. Si ajabu mngepewa hizi taarifa mngezikalia badala ya kuutahadharisha umma, wameona bora wao wautangazie uma kuepusha madhara.

Kuna ubaya gani katika hilo?. Badala ya kukanusha fanyieni kazi hizo rumours.

Wamarekani hawana sababu yoyote ya kutoa taarifa za uzushi.
Eti wanataka kuyumbisha uchumi kwa kutisha wageni. . Uchumi huu huu unaowategemea hao hao Marekani kutusaidia.
Watu wanapenda mizaha sana na usalama wa Watanzania
 
Baada ya Tahadhari ya Usalama katika Jiji la Dar es Salaam katika maeneo ya Masaki na Msasani iliyotolewa na Ubalozini wa Marekani, Mkuu wa mkoa wa Dar amewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari

RC Makonda amesema Jeshi la Polisi linaendelea na kazi kama kawaida kuhakikisha watu wanalala salama na walio kwenye mahoteli wasiwe na hofu ya tishio lolote lile

Aidha, ameomba watoa taarifa kuzigatia sheria, Kanuni na Katiba ya nchi kwani kuna vyombo maalumu vilivyopewa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari
huyu wa la saba mwenzetu vipi?
 
Mnakumbuka Sri Lanka walivyopewa taarifa na India wakapuuza? Kilichofuata ilikuwa ni kulia na kusaga meno.
IGP anasema walikuwa na taarifa. Sasa kwa nini hakutoa tahadhari? Ni vema wananchi wakajua ili wakae macho, watoe taarifa ya kila watakalolishikia shaka.
 
Hawa jamaa sijui vipi? Kwa hiyo mlikuwa mnataka wakae kimya tu wakati intelejensia yao imeonyesha kuna uwezekano wa kushambuliwa?

Yaani badala ya kushukuru mnalaumu. Si ajabu mngepewa hizi taarifa mngezikalia badala ya kuutahadharisha umma, wameona bora wao wautangazie uma kuepusha madhara.

Kuna ubaya gani katika hilo?. Badala ya kukanusha fanyieni kazi hizo rumours.

Wamarekani hawana sababu yoyote ya kutoa taarifa za uzushi.
Hivi ni tahadhali ya kitu gani mkuu?
 
Back
Top Bottom