RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
3,542
2,000
Yote heri tu,,

Nashukuru hawatopata MBAWA ikiwa wamechagua kuwa CHUI...
 

Xheb

New Member
May 18, 2020
4
45
View attachment 1451153

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema hali katika mkoa huo inaendelea vizuri na anachofahamu ni kuwa wamemuomba Mungu na kila mmoja ameendelea kuchukua tahadhari

Amesema “Kila mmoja ameweka jitihada kuhakikisha amevaa barakoa, kwenye daladala tumehakikisha watu wanapeana nafasi, watu wananawa mikono kwa maji tiririka, watu wameendelea kujifukiza na kuchukua tahadhari mbalimbali”

Ameongeza, “Tahadhari hizo zinaleta majibu mazuri na matumaini. Asubuhi nimepokea taarifa kutoka kwa RMO amenambia hali inaendela kuwa nzuri na si mbaya kama ilivyokuwa mwanzo. Watu kupiga simu wamechanganyikiwa imepungua”

Amesema “Mungu anaendelea kutupa neema zake na anatulinda. Nimeona niwape taarifa hii kwa sababu tunapokaa kimya na kuwapa watu waovu nafasi kutumia ukimya wetu kutoa taarifa zisizo sahihi.”

Aidha amebainisha kuwa kuna video moja amefuatilia, watu walinunua majeneza na kwenda sehemu na kujaribu kama kuchimba na kurekodi kuonesha watu wanazikwa usiku. Amesema wapo wanafanya kuonesha hali ni mbaya huku akiomba watu kupuuza taarifa hizo
Duuh😨😨
 
Top Bottom