RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
1,417
2,000
photo_2020-05-13_18-18-26.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema hali katika mkoa huo inaendelea vizuri na anachofahamu ni kuwa wamemuomba Mungu na kila mmoja ameendelea kuchukua tahadhari

Amesema “Kila mmoja ameweka jitihada kuhakikisha amevaa barakoa, kwenye daladala tumehakikisha watu wanapeana nafasi, watu wananawa mikono kwa maji tiririka, watu wameendelea kujifukiza na kuchukua tahadhari mbalimbali”

Ameongeza, “Tahadhari hizo zinaleta majibu mazuri na matumaini. Asubuhi nimepokea taarifa kutoka kwa RMO amenambia hali inaendela kuwa nzuri na si mbaya kama ilivyokuwa mwanzo. Watu kupiga simu wamechanganyikiwa imepungua”

Amesema “Mungu anaendelea kutupa neema zake na anatulinda. Nimeona niwape taarifa hii kwa sababu tunapokaa kimya na kuwapa watu waovu nafasi kutumia ukimya wetu kutoa taarifa zisizo sahihi.”

Aidha amebainisha kuwa kuna video moja amefuatilia, watu walinunua majeneza na kwenda sehemu na kujaribu kama kuchimba na kurekodi kuonesha watu wanazikwa usiku. Amesema wapo wanafanya kuonesha hali ni mbaya huku akiomba watu kupuuza taarifa hizo
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Huyu kiongozi ni "ZERO ZERO ZERO KICHWANI" kabisaaa. Yani kichwa chake kimejaa "MATOPE". Akili zake hua anakua amezikalia. Yani ni punguwani kabisa hili jamaa.

Haya maradhi sio yakufanyia mzaha, ni hatari sana, yapaswa tuyachukulie "SERIOUS" sanaa.

Imefikia hatua nchi zote za jirani zinatuona kama mkaa wa moto. Tanzania tumekua kama vile "WAZALISHAJI/BREEDERS/INCUBATOR" ya COVID-19.
 

Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
1,428
2,000
1)Unapewa habari moja usiyoweza kuithibitisha, inabidi uikubali kwa kuipa benefit of the doubt.

2) unaongezewa habari ya pili ambayo una nafasi kubwa ya kuithibitisha, Na unahisi kwa asilimia kubwa ni uongo.

Inakubudi uamini kuwa zote mbili ni za kutiliwa shaka
 
Top Bottom