RC Makonda hongera kwa jitihada zako, ila nasisitiza tena fanyia kazi haraka hizi kasoro zako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,545
108,873
Nadhani hii si mara yangu ya Kwanza kuja humu JamiiForums na kukusifia kuwa Wewe ni mchapakazi mzuri na mpambanaji wa Kimaendeleo hasa katika huu Mkoa wako wa Dar es Salaam tofauti na watangulizi wako wengi tu ila kuna Kasoro zako ambazo bado naziona zipo na hujaziacha kitu ambacho mara nyingi zinakushusha japo Watu wako wa karibu wanakuficha ila wakikaa wao kwa wao wanakucheka na hata kukudhihaki.

Kasoro yangu kubwa ya kuzaliwa ni ya kupenda kusema ukweli tena kwa Mtu ambaye namheshimu, nampenda na namtakia mafanikio mema bila chembe yoyote ile ya Unafiki au Kupepesa macho au Kutikisa masikio na Kumung'unya maneno nikiwa nategemea kwamba ninavyomsema basi atabadilika na hatimaye kuja kuwa bora zaidi Kiuwajibikaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ( RC ) Paul C. Makonda ukifanyia Kazi ' mapungufu ' yako haya makubwa nakuhakikishia huko mbele utakuja kuwa ' bonge ' la Kiongozi na si ajabu hata hawa ' wanaokubeza ' leo wao ndiyo wakawa sehemu ya Watu watakaokuwa wanakupigia ' chapuo ' na Kukuunga mkono.

Mkuu wa Mkoa Makonda una......

  1. Tabia ya Kukurupuka sana katika mipango yako
  2. Unapenda kutaka upewe Sifa kuliko kufanya Vitu vya Kiuhalisia na vyenye Tija kwa wengi
  3. Tabia kila unapoongea na hadhira / umma ' body language ' yako huwa 100% imejaa dharau na ujivuni kitu ambacho kwa Kiongozi wa Watu si kizuri
  4. Tabia ya Kulazimisha ukubwa hata pasipotakiwa Kuulazimisha
  5. Tabia ya Kuanzisha Kampeni kadha wa kadha lakini zisizo na mwisho mzuri na wenye ufanisi
  6. Tabia ya kupenda sana Kushindana na ' Critics ' wako kitu ambacho mara nyingi kinakuharibia na unajikuta unakosea mno katika mipango yako
  7. Tabia ya kupenda sana kuwa juu ya hata waliokuzidi ' Kiitifaki ' kitu ambacho hakitakusaidia mno na jitahidi ujifunze Kujinyenyekeza kwa hao wakubwa wako wa ' Kiitifaki ' ili waweze kukupa ushirikiano mkubwa kwani wengi wao wanakulalamikia japo ukikutana nao wanakuchekea kwakuwa tu wanajua Wewe una ' influence ' fulani ' mahala ' fulani.
Wewe ni ' bonge ' la Kiongozi tena mpambanaji / mpiganaji kabisa ila yafanyie Kazi hayo mapungufu yako ya ' Kutukuka ' na ipo siku utakuja kuwa na mafanikio makubwa na utanikumbuka GENTAMYCINE kwamba niliwahi Kukushauri / Kukuhusia tofauti na Watu wengi wanaokuzunguka 24/7 ambao ' wanakung'ong'a / wanakusanifu ' tu bila Wewe kujua ila wapo nawe kwakuwa tu unawasaidia kufanya njia zao za Kwenda ' chooni / msalani ' zisiote Nyasi.

Nawasilisha.
 
Kwa mujibu wa maelezo yako wala haumfagilii sema tu inabidi sasa umwambie ukweli huku umejificha nyuma ya sifa feki.Iko hivi huyu bwana ana sifa ya kuwa mpambe wa kiongozi lakini sio sifa ya kuongoza watu.Sio mtu wa kukabidhiwa mamlaka na mtu wa kukaa na kumpamba boss wake ili apaye angalau mlo wa siku the rest ni mambo ya kawaida sana.Sijaone ubonge wa ukiongozi wake zaid ya purukushani za kijana aliyeko kwenye adolescence Ova
 
Acha kunilisha maneno tafadhali na sijakuteua kuwa Msemaji wangu japo naona ni kama vile ' unajipendekeza ' nikupe hilo Jukumu zito na ambalo naamini hutoliweza kwani huna huo uwezo. Na nadhani Wewe utakuwa ni mgeni Kwangu baada ya kutoka huko Kijijini Kwenu Kyaka Nkunde na Ikupilipa Nkoba. Nadhani kama kuna Mtu ambaye yupo katika wale Watu ambao hupenda Kumkosoa ' kavu kavu ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda basi Mimi GENTAMYCINE pia nipo na unaweza ukatafuta humu threads nilizomuanzishia ili ujionee na ujiridhishe.

Sera yangu haijabadilika na haitobadilika ambapo ukifanya mazuri nitakusifia na ukiharibu nitakukosoa bila haya / aibu.
 
Nadhani hii si mara yangu ya Kwanza kuja humu JamiiForums na kukusifia kuwa Wewe ni mchapakazi mzuri na mpambanaji wa Kimaendeleo hasa katika huu Mkoa wako wa Dar es Salaam tofauti na watangulizi wako wengi tu ila kuna Kasoro zako ambazo bado naziona zipo na hujaziacha kitu ambacho mara nyingi zinakushusha japo Watu wako wa karibu wanakuficha ila wakikaa wao kwa wao wanakucheka na hata kukudhihaki.

Kasoro yangu kubwa ya kuzaliwa ni ya kupenda kusema ukweli tena kwa Mtu ambaye namheshimu, nampenda na namtakia mafanikio mema bila chembe yoyote ile ya Unafiki au Kupepesa macho au Kutikisa masikio na Kumung'unya maneno nikiwa nategemea kwamba ninavyomsema basi atabadilika na hatimaye kuja kuwa bora zaidi Kiuwajibikaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ( RC ) Paul C. Makonda ukifanyia Kazi ' mapungufu ' yako haya makubwa nakuhakikishia huko mbele utakuja kuwa ' bonge ' la Kiongozi na si ajabu hata hawa ' wanaokubeza ' leo wao ndiyo wakawa sehemu ya Watu watakaokuwa wanakupigia ' chapuo ' na Kukuunga mkono.

Mkuu wa Mkoa Makonda una......

  1. Tabia ya Kukurupuka sana katika mipango yako
  2. Unapenda kutaka upewe Sifa kuliko kufanya Vitu vya Kiuhalisia na vyenye Tija kwa wengi
  3. Tabia kila unapoongea na hadhira / umma ' body language ' yako huwa 100% imejaa dharau na ujivuni kitu ambacho kwa Kiongozi wa Watu si kizuri
  4. Tabia ya Kulazimisha ukubwa hata pasipotakiwa Kuulazimisha
  5. Tabia ya Kuanzisha Kampeni kadha wa kadha lakini zisizo na mwisho mzuri na wenye ufanisi
  6. Tabia ya kupenda sana Kushindana na ' Critics ' wako kitu ambacho mara nyingi kinakuharibia na unajikuta unakosea mno katika mipango yako
  7. Tabia ya kupenda sana kuwa juu ya hata waliokuzidi ' Kiitifaki ' kitu ambacho hakitakusaidia mno na jitahidi ujifunze Kujinyenyekeza kwa hao wakubwa wako wa ' Kiitifaki ' ili waweze kukupa ushirikiano mkubwa kwani wengi wao wanakulalamikia japo ukikutana nao wanakuchekea kwakuwa tu wanajua Wewe una ' influence ' fulani ' mahala ' fulani.
Wewe ni ' bonge ' la Kiongozi tena mpambanaji / mpiganaji kabisa ila yafanyie Kazi hayo mapungufu yako ya ' Kutukuka ' na ipo siku utakuja kuwa na mafanikio makubwa na utanikumbuka GENTAMYCINE kwamba niliwahi Kukushauri / Kukuhusia tofauti na Watu wengi wanaokuzunguka 24/7 ambao ' wanakung'ong'a / wanakusanifu ' tu bila Wewe kujua ila wapo nawe kwakuwa tu unawasaidia kufanya njia zao za Kwenda ' chooni / msalani ' zisiote Nyasi.

Nawasilisha.
Sijaona ulichozungumza zaidi ya kuzijadili hisia zako kuhusu jambo, na huko ni kuishia kujieleza ulivyo.
Muache dogo apige kazi kwani hatendi ili asifiwe, anatenda kike aonacho ni sahihi kwa masilahi mapana, adui zake ni adui wa masilahi ya umma na ni lazima apambane nayo ili kuzishinda hila zao.
Let his management walk his talk..
 
Acha kunilisha maneno tafadhali na sijakuteua kuwa Msemaji wangu japo naona ni kama vile ' unajipendekeza ' nikupe hilo Jukumu zito na ambalo naamini hutoliweza kwani huna huo uwezo. Na nadhani Wewe utakuwa ni mgeni Kwangu baada ya kutoka huko Kijijini Kwenu Kyaka Nkunde na Ikupilipa Nkoba. Nadhani kama kuna Mtu ambaye yupo katika wale Watu ambao hupenda Kumkosoa ' kavu kavu ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda basi Mimi GENTAMYCINE pia nipo na unaweza ukatafuta humu threads nilizomuanzishia ili ujionee na ujiridhishe.

Sera yangu haijabadilika na haitobadilika ambapo ukifanya mazuri nitakusifia na ukiharibu nitakukosoa bila haya / aibu.
Hata we unapenda sifa

Kweli unayosema
 
Ninachoona sera yako ni kujificha jua kwenye kivuli chako mwenyewe.Unasahau ili uwe na kivuli lazima umulikwe na mwanga wa jua.Ndugu yako DAB anatafutaga kivuli chake gizani mwambie kama vipi awashe taa ndo ataona kivuli
 
Back
Top Bottom