RC Makonda, hebu fanya ziara kwenye vituo vya UDART

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Upatapo ujumbe huu hebu siku moja tembelea vituo vya usafiri vya mwendokasi na wananchi tunaomba ziara hiyo iwe shitukizi, uje ujionee wasafiri tunavyopangwa foleni ndefu huku tukisubiri gari hadi saa nzima wakati mwingine ili hali hapo kituoni kuna gari nyingi mno zimepark! Gari zinazofanya Safari ni chache mno abiria tupo wengi na tumeshalipia nauli.

Jaribu uzungukie japo vituo vyote vikubwa na ikibidi usikilize comments zetu abiria na tungependa maoni yetu yasipuuzwe bali yafanyiwe kazi na serikali . Sijui tatizo lipo wapi? Madereva? Gari au usimamizi?
 
Tena abiria wa vituo vya kati kati mfano bucha na barut waweza kaaa kituon masaa mawili ukisubir bus.
 
Kwanini msipande daladala za kawaida, mbona hazina hayo maujinga? Inashangaza watu mmejazana mwendokasi pale kimara wakati pembeni tu kunankituo Cha Mabasi ya kawaida yanasubiri abiria
 
Kwanini msipande daladala za kawaida..mbona hazina hayo maujinga? Inashangaza watu mmejazana mwendokasi pale kimara wakati pembeni tu kunankituo Cha Mabasi ya kawaida yanasubiri abiria
Hizo safari za daladala zimeruhusiwa tu wakati huu wa corona, hakuna daladala inayofanya kazi kwenye route zote za mwendokasi.
 
Kwanini msipande daladala za kawaida, mbona hazina hayo maujinga? Inashangaza watu mmejazana mwendokasi pale kimara wakati pembeni tu kunankituo Cha Mabasi ya kawaida yanasubiri abiria
Huu ni usafiri wa haraka mtu una uhakika ndani ya dkk 18/20..upo mjini
Tatizo waendeshaji ndio wanazingua
 
Back
Top Bottom