RC Makonda hakukata tamaa kwenye safari yake ya mafanikio

Sauti ya Rondo

Senior Member
Aug 1, 2009
127
250
Siku zote Makonda ameeleza kwenye vituo vya Redio na TV kuwa yeye ni mtoto wa masikini na hata wazazi wake ni masikini ila hakukubali umasikini huo ufifishe ndoto yake na ndiyo maana anafanya kazi kwa bidii na kujituma huku akiwapigania wanyonge na masikini.

Katika muda mfupi wa utumishi wake wa umma tumeshuhudia akisimamia ujenzi wa ward tatu za kisasa kwa ajili ya akina mama, ICU ya kisasa, Ujenzi wa barabara, Hakuishia hapo tu mpaka kwenye elimu hata sina sababu ya kuelezea kwanini Makonda anakwenda kila kona.

Ila la msingi hapa aliweka jitihada. Huu ni wakati wa kuitazama picha hiyo inayosambazwa na wabaya wake kupotosha agenda zake mbalimbali za kuboresha maisha ya wana DSM kama picha ya kumtia moyo yeye na kuwatia moyo watoto wote wa masikini na wanyonge wasikate tamaa kwani siku moja ndoto zao zitatimia.

Ila lazima wawajibike na kuweka bidii kama Makonda na zaidi ya hapo.

Screenshot from 2016-07-20 17:18:28.png
 

mndorwe

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
2,476
2,000
Tatizo ni matamshi yake watu walikuwa wanamkumbusha asisahau alikotoka na kuanza kuwadharau wasio na ajira...et atawasaka....
 

Moro¹One¹

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
504
1,000
Umasikini wake huko alikotoka haimaanishi afunge Mdomo asiwazungumzie Wazurulaji, ajira utafutwa kwa Malengo, ndio maana ata yeye Makonda alitoka chini akaenda juu. Watu hawataki kutafuta kazi, pia kufanya kazi kwa kujitoa ili watu waone uwepo wako wakusaidie, kama uangaiki uwezi fika na kupata kitu. Muacheni Mkuu wa Mkoa aonyeshe jinsi ya vijana tunapasa kuishi. Piga kazi Mkuu wa Mkoa Makonda, Mafanikio uwafuata walio jasiri sana( Ufalme wa Mungu uridhiwa kwa Walio na nguvu) By Jesus Christ.
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,671
2,000
Huyu ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Makonda
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1469029883349.jpeg
    File size
    83.6 KB
    Views
    34

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,632
2,000
makonda kaingia jijini mwaka 2009 kwa mara ya kwanza so anatakiwa kujifunza mila ,desturi,tamaduni na taratibu za watu wa pwani.mwalimu nyerere mwenyewe alipokuja dar kwa mara ya kwanza miaka ya 1950 enzi hizo akivaa kaptula akakutana na watoto wa mjini akija sykes ,dossa aziz,kiyate na wenzake ilibidi achukue muda kusoma tamaduni zao mpaka alipolijua jiji ,sasa huyu kaja juzi tu anakuja na speed ya mwendo kasi kwenye jiji la watudar watu hawalimi wala hawavuni hawana kazi wala biashara nani huwalisha,?
 

cantonna

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,123
1,500
Umasikini wake huko alikotoka haimaanishi afunge Mdomo asiwazungumzie Wazurulaji, ajira utafutwa kwa Malengo, ndio maana ata yeye Makonda alitoka chini akaenda juu. Watu hawataki kutafuta kazi, pia kufanya kazi kwa kujitoa ili watu waone uwepo wako wakusaidie, kama uangaiki uwezi fika na kupata kitu. Muacheni Mkuu wa Mkoa aonyeshe jinsi ya vijana tunapasa kuishi. Piga kazi Mkuu wa Mkoa Makonda, Mafanikio uwafuata walio jasiri sana( Ufalme wa Mungu uridhiwa kwa Walio na nguvu) By Jesus Christ.
Hivi wanaozurula unafikili wanapenda ww??
 

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,273
2,000
Watu huku Pwani tunayo misukule, chuma ulete hii yote inatuingizia kipato Mkuu, usituone tunacheza bao tuu ukazani ni wazurulaji.

Tusiingiliane kazi bnaa, mnaweza mkaingia nyumba ya MTU kufanya msako wenu mkatoka nduki wenyewe bila kuaga. Watu tunaitwa Maprofesa lakini hata kidato hatukijui.

Ajabu hata hao maprofesa wenu waliosoma mpaka nywele zikayeyuka kichwani wanakuja kwetu Maprofesa maji marefu tuwasaidie.

Haa haa haaa natania tuu Mazee bongo ndumba hazifanyi kazi zaidi ya Akili yako tuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom