RC Makonda atembelewa na wawekezaji kutoka China, viwanda 200 kujengwa

Donatila Sqm million tano Dar es Salaam?? Viwanda 200 Dar es Salaam? Wanajenga viwanda Kunduchi?

Wawekezaji wanaenda kuwekeza Tanga wanapokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam??

Huyu jamaa mbona anapewa promo kuliko hata mawaziri waandamizi!?
 
Sqm million tano Dar es Salaam?? Viwanda 200 Dar es Salaam? Wanajenga viwanda Kunduchi?
Wawekezaji wanaenda kuwekeza Tanga wanapokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam??

Huyu jamaa mbona anapewa promo kuliko hata mawaziri waandamizi!?

Sio promo wakuu wa mikoa wote wamepewa target ya kuwa na viwanda 100 kila mkoa na waziri wa Tamisemi na serikali za mitaa.Yeye kaenda china kuwatafuta wawekezaji kwa ajili ya mkoa wake sasa kosa lake liko wapi? Acheni kijana apige kazi....Bravo Makonda
 
Nanyie acheni kubeza zuhudi za wenzenu ni juzi tu mikataba imesainiwa alafu leo hii unataka uone viwanda tayari vinafanya kazi? Sisi tumekaa tangu tupate uhuru miaka zaidi ya 50 hatujaweka viwanda alafu unalaumu wenzio walioleta wazo la viwanda miaka miwili tu iliopita? Tutakalia kubeti tu pesa ya chapchap.
 
Hizi drama tu kama bongo movie lakini hakuna lolote la maana.

Hivi zile mikataba kibao za yule Mmorocco walizosainigi serikali ukiwamo uwanja mkubwa wa michezo Dodoma zilifiaga wapi?

Alikujaga hapa rais wa China tukaambiwa serikali imetiliana saini makubaliano ya mikata kibao kama 21 ya maendeleo, nayo ilifiaga wapi?

Alikujaga Obama na yeye wakasaini mikataba kibao na serikali, nayo ilijifiaga wapi?

Kila viongozi wa nchi mbalimbali wakija hapa nchini huja na makubaliano ya kusaini mikataba kibao lakini mwisho wa siku hakuna linalofanyika nyuma yake.
Nanyie acheni kubeza zuhudi za wenzenu ni juzi tu mikataba imesainiwa alafu leo hii unataka uone viwanda tayari vinafanya kazi? Sisi tumekaa tangu tupate uhuru miaka zaidi ya 50 hatujaweka viwanda alafu unalaumu wenzio walioleta wazo la viwanda miaka miwili tu iliopita? Tutakalia kubeti tu pesa ya chapchap
 
Huyu
455e5ceb55b599203b9cd6538cc06147.jpg
huyu hakuna kitu asichoweza kukiangalia bila kujaribu...ispokuwa
Alishindwa kujaribu ile kitu ile siku ya kusajili.
b95dbf02ca5be4ccca9a5fc0119c9caf.jpg
5dbbcac2ba35a93955a392b004c5482d.jpg
2d0e0d887e5b97bc1cf267973a04a3ba.jpg
cdb4e316415f0aebe9550862ebeccb03.jpg
Unatunza kumbukumbu na ile anataka pilau la ramadhani

Sent from my HUAWEI G6-U10 using JamiiForums mobile app
 
hivi kwa nini msiboreshe viwanda vilivyopo? mfano mzuri kiwanda cha Urafiki. kile kingeboreshwa chote kingetoa ajira kubwa sana hapa nchini na swala la nguo za mitumba tungesahau. mngeweka mitambo mipya, miundo mbinu mpya, management mpya, mngechukua wataalam kutoka nje waje watupe shule kuhusu kutengeneza nguo nzuri kama hizi tunazozitoa nchi zilizoendelea.

badala ya kuanzisha kitu kipya tungeboresha hivi vilivyopo na kuviingiza kwenye ushindani wa kimataifa.
 
Hizi drama tu kama bongo movie lakini hakuna lolote la maana.

Hivi zile mikataba kibao za yule Mmorocco walizosainigi serikali ukiwamo uwanja mkubwa wa michezo Dodoma zilifiaga wapi?

Alikujaga hapa rais wa China tukaambiwa serikali imetiliana saini makubaliano ya mikata kibao kama 21 ya maendeleo, nayo ilifiaga wapi?

Alikujaga Obama na yeye wakasaini mikataba kibao na serikali, nayo ilijifiaga wapi?

Kila viongozi wa nchi mbalimbali wakija hapa nchini huja na makubaliano ya kusaini mikataba kibao lakini mwisho wa siku hakuna linalofanyika nyuma yake.
Hapo sasa ......... na Waziri Mkuu wa Ethiopia na Cargo Hub Tanga .............!!

Zuma wa RSA na mkopo wa SGR ...................

Siku tukiwa Donor country na mimi nitawekeza ..............!!
 
China angetusaidia kwenye migodi ya mkaa wa mawe na ufuaji wa umeme toka kwenye mkaa wa mawe.

Lakini ingependeza zaidi China kujikita kwenye Heavy Industries kama kufua chuma yaani iron ore na mazao yake.

Ili nchi iwe ya viwanda chuma na mkaa wa mawe havikwepeki.Matumizi ya chuma na mazao ya chuma ndio haswa nguzo kuu ya viwanda.

Lakini jambo la kushangaza kuna sintofahamu ya NDC alietumia pesa zetu zaidi ya miaka 40 tokea enzi za Mwl.Nyerere hakuwai kujenga kiwanda cha iron ore. Labda tupimwe mkojo tunamatatizo.
 
Hizi drama tu kama bongo movie lakini hakuna lolote la maana.

Hivi zile mikataba kibao za yule Mmorocco walizosainigi serikali ukiwamo uwanja mkubwa wa michezo Dodoma zilifiaga wapi?

Alikujaga hapa rais wa China tukaambiwa serikali imetiliana saini makubaliano ya mikata kibao kama 21 ya maendeleo, nayo ilifiaga wapi?

Alikujaga Obama na yeye wakasaini mikataba kibao na serikali, nayo ilijifiaga wapi?

Kila viongozi wa nchi mbalimbali wakija hapa nchini huja na makubaliano ya kusaini mikataba kibao lakini mwisho wa siku hakuna linalofanyika nyuma yake.
Ongezea na yule waziri mkuu wa India alikujaga bongo wakasaini mikataba kibao + wakulima wakaambiwa walime mbaazi kuna soko la uhakika...matokeo yake mwaka jana India wamegoma kununua mbaazi yetu
 
China angetusaidia kwenye migodi ya mkaa wa mawe na ufuaji wa umeme toka kwenye mkaa wa mawe.
Lakini ingependeza zaidi China kujikita kwenye Heavy Industries kama kufua chuma yaani iron ore na mazao yake.
Ili nchi iwe ya viwanda chuma na mkaa wa mawe havikwepeki.Matumizi ya chuma na mazao ya chuma ndio haswa nguzo kuu ya viwanda.
Lakini jambo la kushangaza kuna sintofahamu ya NDC alietumia pesa zetu zaidi ya miaka 40 tokea enzi za Mwl.Nyerere hakuwai kujenga kiwanda cha iron ore.Labda tupimwe mkojo tunamatatizo.

Kiwanda cha chuma kingekuwa ni moja ya kipaumbele kwa kiasi kikubwa kingesaidia..
Kenya Tayari wanajenga zaidi ya 500W plant lakini target yao hasa nafikiri ni coal kutoka Tanzania..

Reserve ya coal tunayo lakini mpaka sasa ni underutilized wakati tungeweza hata kuweka COAL FIRED PLANT plant Songea yenye uwezo wa hata 500MW na south coridor yoote ikalishwa na hiyo plant na Gas ikabaki standby plat pale Mtwara.

Sijui nani katuroga..
 
Wazo la viwanda ni zuri lakini njia za kufikia uchumi wa viwanda bado ni duni.

Maendeleo ya viwanda hayaji kwa kutumia wawekezaji kutoka nje, maendeleo ya viwanda hufanywa na wawekezaji wa ndani baada ya kuwa na mitaja na teknolojia, Maendeleo ya viwanda yangeanzia na serikali yenyewe kuwekeza kwenye rasirimali watu kwa watu kujifunza teknolojia na kuwa na mitaji.

Hakuna Taifa liliondelea kwenye teknolojia ya viwanda kwa kutegemea mitaji ya wawekezaji kutoka nje, kwa kuanzia huwezi kutegemea mitaji ya watu kutoka nje bali unatakiwa uanze kuwekeza mwenyewe na kuchangamsha mzunguko ambao watu wengine mwisho wasiku wataufuata na kuja kuwekeza mitaji..

China alijifunza teknolojia kwanza na kuwekeza kwenye rasirimali watu ambao walichangamsha mzunguko wa kibiashara ndani ya China na wawekezaji wakichina walipopata mitaji walitoka nje kuwekeza kiasi cha kuvutia wawekezaji wageni kutoka nje kukimbilia China kuwekeza wakiwa na uhakika wa rasirimali watu na teknolojia na mwisho wa siku gharama ndogo za uzalishaji
 
Donatila Paragraph yako ya pili kutoka mwisho umekosea kwani alisema ''kuna clip inyozunguka mitandaoni Ethiopia ina Inastrial park kubwa kuliko zote Afrika na kusema yetu itakuwa kubwa kwa kuliko zote akataja mita za mraba ambazo ni ml 5''
Sio kiwanda ni industial park
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom