RC Makonda atembelea mradi wa ujenzi wa njia nane kutoka Morocco hadi Mwenge

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara nne mpya kutoka Morocco hadi Mwenge ambapo kukamilika kwa njia hizo kutafanya idadi ya barabara kufikia nane jambo linalotarajiwa kupunguza na ikiwezekana kumaliza tatizo la foleni kwenye barabara ya Bagamoyo.

RC Makonda amesema barabara hiyo ina urefu wa Km 4.3 na itagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 79 hadi kukamilika ikihusisha uwekaji wa Taa za barabarani, Vivuko, Mitaro, Sehemu ya kufanyia mazoezi na eneo la watembea kwa miguu ambapo ujenzi huo unaenda sambamba ujenzi wa Mferegi mkubwa na wakisasa wa kusafirisha maji ya mvua kutoka Shekilango, maeneo yote ya Sinza, Mwenge, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama kupitia Mikocheni eneo la Tanesco na kuyapeleka hadi baharini jambo litakalosaidia kumaliza kero ya maji kipindi cha mvua.

Aidha RC Makonda amesema katikati ya barabara hiyo kumeachwa kwaajili ya Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi huku akimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa namna anavyozipatia majibu kero za wakazi wa Dar es salaam.

Pamoja na hayo RC Makonda pia amesema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa Service Road yenye upana wa Mita 6.5 kuingilia Stand mpya ya Mwenge kutokea Bamaga pamoja na kuunganisha barabara za Sinza mapambano, barabara ya nyuma ya chuo cha ustawi wa jamii kutokea barabara ya akachube.

Hata hivyo RC Makonda amesema upanuzi wa barabara ya njia nne kutoka Shekilango hadi Bamaga unatarajiwa kuanza siku yoyote kuanzia sasa kwakuwa fedha zipo.

Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea pia Mradi wa Ujenzi Wa Barabara na Mitaro ya Maji ya Mvua Eneo la Bwawani kata ya Mwananyamala ambalo Kwa muda mrefu wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiteseka na kero ya maji kujaa na kutwama katika makazi yao lakini Kwa sasa wakazi wa eneo hilo wanafurahia barabara nzuri na mitaro ya kisasa ya kupitisha maji.

TUKUTANE SITE 2019.
 
Hongera Magufuli kwa kujali Watanzania
Endelea kuchapa kazi

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao
 
79,000,000,000/= kwa 4.3km hapa napata homa, kwahiyo Dodoma hatuendi Tena?
 
Hii pesa hapana Kuna namna hata barabara za Laxernburg sio aghali hivi! Kwahiyo kutakuwa na reli ya umeme?
 
barabara hiyo ina urefu wa Km 4.3 na itagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 79 hadi kukamilika ikihusisha uwekaji wa Taa za barabarani, Vivuko, Mitaro, Sehemu ya kufanyia mazoezi na eneo la watembea kwa miguu ambapo ujenzi huo unaenda sambamba ujenzi wa Mferegi mkubwa na wakisasa wa kusafirisha maji ya mvua kutoka Shekilango

Yetu macho
 
Back
Top Bottom