OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,567
Wakuu napenda kuwapa uelewa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar asipimwe kwa kuuza sura kwenye TV na Radio,apimwe kwa utendaji wake na accomplishment of plans.
Niwape taarifa kuwa ni mwaka sasa umeisha RC Makonda ameshindwa kuitisha vikao vikubwa viwili katika Mkoa wake.Ajabu anachukuliwa kama mtendaji bora wa nchi hii.
Kikao cha kwanza ni RCC hiki ni kikao cha Mashauriano ya Mkoa ambacho ni kwa ajili ya kuangalia na kutathmini maendeleo ya Mkoa mzima,ambapo mkuu wa Mkoa hufanya kikao yeye na wawakilishi wake ngazi ya Mkoa mpaka wilaya.Kikao hiki kinajumuisha wadau wa maendeleo wa Mkoa,wabunge,masharika muhimu ndani ya Mkoa kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mkoa.RC Makonda ameshindwa kuitisha kikao lakini amepata mda na rasilimali za kufanya party
Kikao kingine ni Kikao cha Mfuko wa barabara. Hiki ni kikao cha kipekee kabisa,kinachojadili mashaka yote ya miundombinu ya barabara katika Mkoa,ambacho kinakuwa na wadau muhimu kama wabunge,wakurugenzi wa manispaa na Tanroads. Mkuu wa Mkoa hajaona umuhimu wa vikao hivi ameona apige party tena mida ya kazi