RC Makonda anatumia msafara wa magari zaidi ya 35

Kama kama upuuzi wa kiwango cha kusikitisha ni wa makonda jioni ya leo akiwa kwenye kitu kinachoitwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Nikiwa niko Jof pub njia ya ubungo maziwa nilishuhudia msafara wa magari yasiyopungua 35 yakiwemo ya jeshi la polisi trafiki na ffu yote yakiwa full loaded.

Gari nyingine zote hazikupungua watu wane!hakukuwa na gari ndogo hata moja VX V8 zilikuwa tano! Shangilieni huu upuuzi lakini mjue hiki kiama ni chetu sote....
Amepewa support
 
Nini mnaongelea humu? Heading haieleweki, content ndio nonsense kabisa, senseless rubbish! Tuache kulalamika kama wanawake
Wanawake ni pamoja na mama yako. Kwa tafsiri yako, maneno uliyoandika siyo hoja, ni ya kulalamika lalamika. Hivyo wewe ni mwanamke.
 
Kama kama upuuzi wa kiwango cha kusikitisha ni wa makonda jioni ya leo akiwa kwenye kitu kinachoitwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Nikiwa niko Jof pub njia ya ubungo maziwa nilishuhudia msafara wa magari yasiyopungua 35 yakiwemo ya jeshi la polisi trafiki na ffu yote yakiwa full loaded.

Gari nyingine zote hazikupungua watu wane!hakukuwa na gari ndogo hata moja VX V8 zilikuwa tano! Shangilieni huu upuuzi lakini mjue hiki kiama ni chetu sote....
CCM niliwapa wazo LA kukodi mabasi aina ya Eicher ili kubana matumizi wamegoma. Halafu wanaendelea kuwadanganya Watanzania kuwa wanabana matumizi.
Hizi hela za posho kwa madereva na watumishi wengine kwenye hizo ziara, gharama za mafuta na za uchakavu wa vyombo (depreciation) CCM wamezifumbia macho.
CCM ni ileile
 
alishasema kafadhiliwa haina shida kiongozi atakiwi kukaa ofisini kuletewa taarifa za kupikwa atadanganywa,huwezi lima Shamba Kwa simu lazima uende.
 
Sikujua kama huyu jamaa mleta mada ni mmbea hivi! Mwanaume mzima na akili zake anaanza kuhesabu magari kisa tu apate la kuongea. Ni majungu na umbea wa hali ya juu, kaa chonjo utavalishwa khanga muda si mrefu. Pia post yako imejaa lugha isiyo ya staha hata kidogo, take care!
 
Ningependa nimuone mh. Rais akimhamishia Makonda kati ya mikoa ifuatayo ili akachape kazi na kuwaondolea wananchi umaskini na sio kubaki DSM na siasa za vyomba vya habari wakati kila mtu Dsm anajua kilichompeleka jijini hata kama pangekua hakuna utawala wananchi wangeendelea na maisha yao kama kule Mogadishi tu.
Ampeleke mikoa kama :-
Dodoma
Lindi.
Singida .
Tabora
Kigoma ,
Shimiu.
Shinyanga.
Tanga.
Pwani.
Rukwa.
Kagera.

Aende huko ambapo wananchi hawana hata maji safi yakunywa.Mikoa ambayo hata vyoo vya shimo ni tabu.
Mikoa iliyojaa migogoro ya ardhi na umaskini wa kipato.
Sasa nashangaa Mkuu anamsifia Makonda kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wenzake wakati amekaa mkoa ambao unamzunguko mkubwa wa fedha na wafanyabiashara wa kila aina.
Dsm ni mkoa mdogo kama wilaya moja tu ya Kasulu ,tena ukiwa na miundo mbinu mizuri.
Sasa imefikia mahali pa kuona uwezo wa makonda kwa kumpeleka mkoa maskini sana ili asikilize na kutatua kero za wananchi.
 
Back
Top Bottom