RC Makonda anatumia msafara wa magari zaidi ya 35

Kama kama upuuzi wa kiwango cha kusikitisha ni wa makonda jioni ya leo akiwa kwenye kitu kinachoitwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Nikiwa niko Jof pub njia ya ubungo maziwa nilishuhudia msafara wa magari yasiyopungua 35 yakiwemo ya jeshi la polisi trafiki na ffu yote yakiwa full loaded.

Gari nyingine zote hazikupungua watu wane!hakukuwa na gari ndogo hata moja VX V8 zilikuwa tano! Shangilieni huu upuuzi lakini mjue hiki kiama ni chetu sote....
Mshana ulitaka awe na gari ngapi.....!!!?
 
kazi ya kusikiliza kero za watu ni kazi ya wabunge na madiwani sasa mkuu wa mkoa anapofanya kazi hizo anataka madiwani na wabunge wafanye nini??[/QUOTE
Kinachoshudiwa ni kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu" katika utekelezaji wake. Utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi uliasisiwa na rais mtaafu mhe Ali Hassan Mwinyi. Alitenga siku na pakawepo mahala ambapo wananchi walimfuata kueleza kero zao. Rais Mtaafu hakufanya misafara ya kwenda kutafuta kero! Mtindo wa kuongozana na msururu wa magari ya watendaji haufai kwa vile:

1. Misafara inaongeza msongamano wa magari sehemu inakopita mbali na gharama za matumizi mabaya ya magari na mafuta, na
2. Kusikiliza kero hakuna tija kwa sababu:
(a) kero za Dar ni nyingi zikiwemo zinazofahamika za upatikanaji maji, ubovu wa barabara, makazi duni, huduma duni za afya, nk.
(b) rc na serikali hawana uwezo wa kuzitatua.
Njia muafaka wa kuendesha nchi kuweka mfumo (system) uliosukwa vizuri unaowezesha utekelezaji wa masuala kuanzia ngazi ya juu hadi ngazi ya chini. "One man's show" ni mtindo mbovu kabisa unaofanya kazi kwa kutegemea uwepo wa mtu. Mtindo huu si endelevu na haupaswi kutumiwa kuendesha mkoa wala nchi.

Utendaji kwa mtindo wa mtu mmoja mmoja au one man's show unalenga kumpatia mhusika umaarufu usiokuwepo na kuwatia gazi wenye kero.
Wanaomuunga mkono mhe Paul Makonda kwa jinsi anavyoongoza mkoa wa Dar wanadai anafanya kazi nzuri ila watu wana chuki binafsi dhidi yake na wanamuonea wivu. Wapo wasiokubaliana na madai hayo.

Mkoa wa Dar es salaam umekuwa na wakuu wa mkoa wangapi tangu tupate Uhuru? Kandoro, kwa mfano, alifanya vizuri kama RC bila makeke, kihere, kimbelembele wala mbwembwe. Alikuwepo mzee wa mistari na mhamasishaji, Yusufu Makamba, nk.

Mhe Makonda aliongezewa unga na aliyemteua kwa kuona kazi yake nzuri akiwa DC. Aliipenda kazi yake. Wanaodhani anafanya vibaya na kuwa ni jipu tarajiwa, wasahau.

Tanzania ni kisiwa cha amani. Ni nchi tajiri kwa mambo mengi ila maskini wa utawala bora. Viongozi wana Uhuru wa kutamka na kufanya yanayowaijia vichwani mwao. Nailinganisha gari lililokosa matairi. Je, tutafika huko tunaokotarajia kufika?

 
1480213970614.jpg
 
Duh! mukulu haoni hili..? au anaacha jipu liive!
Kwa mkulu hili sio jipu eti ndio uchapa kazi hukusikia yale maigizo yao kwenye Simu? Atakaye chagua au kifadhili CCM Mungu amlaani na kizazi chake chote mpaka mifugo yake yote.
 
hakupiga hata simu kwenye wahanga wa Bukoba na masikini wasio na sauti akala pesa za rambirambi za wahanga bukoba Mungu anawaona.


swissme
si ndo hapo sasa, yani hats serikali ifanye nini ila swala la kula rambi rambi haliwezi futika kichwan mwa watanzania, na huko tunapoelekea ipo siku mtu yuko jukwaani akisema "hapa kazi tu" "wanao lalamika ni wapiga dili" atarushiwa chupa za mikojo na mawe, huu ungese umezidi sasa.
 
Back
Top Bottom