RC Makonda amuomba radhi Rais Magufuli na watanzania wote kwa kipigo ilichopata Taifa stars

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,766
141,630
Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Taifa stars RC Makonda amemwomba radhi Rais Magufuli na watanzania wote kwa ujumla kwa kipigo ilichopata kutoka kwa Harambee stars.

Makonda amesema mpira ni dakika 90 na ndivyo ilivyotokea Cairo jana lakini hata hivyo mechi ya jana vijana wetu walicheza vizuri kuliko siku ya Senegal.

Makonda amesema wananchi wanapaswa kuipenda timu ya Taifa badala ya kuibeza.
Mwisho Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kumtuma Cairo Misri kuiongezea nguvu Taifa stars na kwamba yeye ( Makonda) anarejea nyumbani lakini anaamini vijana wetu wataigaragaza Algeria katika mechi yao ya mwisho.

Source Global publishers tv
Maendeleo hayana vyama!
 
Waache kutuletea siasa zao zisizo na manufaa kwa mustakabari wa Taifa letu. Mbona Burundi nayo imefungwa mechi zote mbili! kwa sababu jambo hilo ni la kawaida sana kwa timu ambayo haikujiandaa na ambayo imekosa viwango vya kiushindani!

Matamko ya kuomba radhi kwa nini yasitolewe na TFF au benchi la ufundi kama ilivyotokea kwa Serengeti boys ilipovurunda kwenye afcon ya vijana mwaka huu 2019? Jambo la msingi ni kujipanga kwa vitendo na kurudi kwa kishindo. Uwekezaji haukwepeki! Na pia kuna umuhimu wa kuruhusu uraia pacha! Ccm iachane na uwoga wa kipuuzi.
 
Mkuu hawa wanasiasa dhamira yao ni kuharibu ktk michezo tu, sidhani kama wana jambo jema zaidi ya cheap popularity.
What a shame!!!
 
Back
Top Bottom