RC Makonda aibuka tena na Tezi Dume”Hata ukisafiri Dodoma,tutakufata upimwe

FCR

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
213
177
Mkuu wa mkoa wa daresalaam Leo katika kipindi Cha EATV ametangaza kuwa ndani ya mwaka 2019/2020 hataki kuona viongozi watakao chaguliwa kuwa na tatizo Hilo la tezi dume hivyo kufuatana na maneno hayo amesema kwamba kila mmoja atapimwa kwa lazima siyo ombi huku akibainisha kuwa yeye Kama mkuu wa mkoa ni jukumu la kuwalinda wananchi wake hata hivyo ameenda mbali kwamba Kama wakati wa upimaji utakimbia mkoa na kuelekea dodoma watakufuata hukohuko uliko lengo kubwa 2020 kupata viongozi wenye afya njema ili wawatumikie vizuri wananchi wao!

=====

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema anataka mpaka kufikia Uchaguzi Mkuu 2019/2020 wakazi wa Jiji la Dar es salaam wakiwa wanashiriki zoezi hilo la kuchagua viongozi wakiwa hawana ugonjwa wa tezi dume.
makondaaaaa.jpeg

Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda​
Paul Makonda ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam ambapo amesema nia yake kama Mkuu wa Mkoa ni kuhakikisha wananchi wa Mkoa wake wakiwemo wanaume na wanawake wanapima ugonjwa tezi dume.
Makonda amesema, "nadhani mwaka huu ndiyo sahihi wa kuendesha zoezi la upimaji wa tezi dume, nataka wanaume na wanawake wote tunaenda uchaguzi wa 2019, 2020 hakuna tezi dume."

"Kama wewe ni mwananchi wa Dar es salaam na unaelekea Dodoma tutakufuata huko hatutaki uende mkoa mwingine ukiwa unaumwa, niwaombe wananchi wa Dar es salaam wajitokeze kupima na usipokuja tutakufuata nyumbani kwa sababu ni jukumu letu kukulinda", ameongeza Makonda.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuna yule mwingine huko Mbeya nimesikia amesema mume akichepuka apelekewe taarifa atashughulika na mchepukaji.

Hawa watu wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Anthony Mtaka.

Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwapuuza wale wenye majungu waliomwambia Mtaka hafai hata kuwa mkuu wa wilaya.
 

Kuna yule mwingine huko Mbeya nimesikia amesema mume akichepuka apelekewe taarifa atashughulika na mchepukaji.

Hawa watu wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Anthony Mtaka.

Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwapuuza wale wenye majungu waliomwambia Mtaka hafai hata kuwa mkuu wa wilaya.
Unajua ni watu gani walimwambia hivyo?
 
Wasisahau kupima na malinda.Pia huu ni mwaka wa tathimini za majuihisho ya ahadi zake,matamwa yake yote.Pia akumbuke jiji bado ni chafu, mwendikasi ni shida,machangudoa na mateja bado wamejaa, jiji lake ndo laongoza kwa wasiojulikana vipi juu ya usalama wa wakazi wake anatuahidi nn,ttzo La MAJI bado lipo,uchafu kila kona, elimu imeshuka sana,ana mikakati IPI ya kuondoa kero za jiji
 
Back
Top Bottom