RC Makonda afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa ofisi za BAKWATA

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
3fada2a12fd8d657a5621679dccde7eb.jpg
af89ed76da1f673cb651e5bf38b8f504.jpg


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akifuatana na Mufti wa Tanzania sheikh abubakar zubairy bin Ally, wamefanya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Ghorofa nne la kisasa litakalokuwa ofisi za Baraza kuu la Waislamu nchini katika viwanda vya (BAKWATA) kinondoni jijini Dar es salaam

Ujenzi wa jengo hilo unatarajia kukamilika Juni mwaka 2017 ambapo ofisi zake zitakuwa katika hadhi ya kimataifa ambapo kiasi cha shilingi bilioni 5 chini ya ufadhili wa GSM Foundation zitatumika katika ujenzi huo baada ya Mkuu wa mkoa wa DSM kuahidi ujenzi wa ofisi mpya za Bakwata

Makonda akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo alisema anaridhishwa na kasi ya ujenzi wa ofisi hiyo lakini pia ndoto yake ya kutaka viongozi wa dini wawe katika ofisi zenye hadhi na zenye kuheshimika
719d55f5652c0583e161147a403ddabf.jpg
Mkurugenzi wa Mradi huo Injinia Hans Said amesema ujenzi huo unaendelea vizuri na wamekamilisha ghorofa ya kwanza na kuahidi kuwa baada ya wiki mbili watakuwa wamekamilisha ghorofa ya pili kutokana na kasi inayoendelea ya ujenzi huo.
 
vipi zile shule za Uingereza Bukoba nazo zimefikia coz ngapi?
 
Its simple hii pesa ya gsm ila jamaa anijifanya yy ndio kaitfta bongo bwana kwnn lema haya maono hamkuota huyu kijna
 
Makonda anajiandalia njia ya kuja kugombea Uraisi miaka 15 ijayo
 
Huyu GSM ni nani? Wadau mnijuze Tafadhali!
Ni mtaalamu wa kuwapiga chenga TRA nasikia alipiga bonge la dalizi kabla TRA hawajashtuka akawapiga tobo ngoma ikaibuka GSM

Ni mchezaji wa kimataifa alitikisa sana enzi ya JK sasa hivi amebadili namba anacheza kama beki mtakatifu anapiga but za hapa na pale huku akimcheki refa
 
Former "Home Shopping"

Kumbuka wakati wa mfungo wa Ramadhani Makonda alikaribishwa kufuturu kwa huyu jamaa wa Home Shopping Center.. Inawezekana tayari lilishazaliwa wazo hili, maana baadae ndio Makonda alizungumzia suala la Bakwata kuwa na jengo lao..
 
Kumbuka wakati wa mfungo wa Ramadhani Makonda alikaribishwa kufuturu kwa huyu jamaa wa Home Shopping Center.. Inawezekana tayari lilishazaliwa wazo hili, maana baadae ndio Makonda alizungumzia suala la Bakwata kuwa na jengo lao..

Nakumbuka mkuu, na hapo ndio maswali yanaanzia - hawa jamaa wa GSM Foundation ni wa-Islam na pengine wanaswali hata msikiti mmoja na Mufti! Kama nia yako ni sadaq/zakat kwa nini hawakumalizana na Mufti huko huko kwenye viunga vyao na badala yake wanamtumia Makonda kama mshenga - mtu ambaye ni mwanasiasa tena kafir?
 
Mchezo Huu Unataka Akili Kubwa Sana Kuelewa
Hata Anayesema Acha Niinyooshe Nchi Hajaelewa Huu Mchezo Maana Naye Kazunguukwa Hata Alipokuja Mfalme.

GSM GROUP OF COMPANIES Ndiyo Kupe Kubwa Sana
Ambapo Lina Jina Jipya
 
Back
Top Bottom