RC Makonda afanikisha safari na matibabu ya Ahmed Albaity nchini China

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
MAKONDA AFANIKISHA SAFARI NA MATIBABU YA AHMED ALBAITY CHINA

makonda-1.jpg

NDOTO na shauku ya kijana Ahmed Albaity alieteseka kwa zaidi ya Miaka 10 Kitandani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu leo imebadilika kuwa furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kumkabidhi Tiketi za Ndege za watu Wanne kwaajili ya safari ya kwenda kupatiwa matibabu Nchini China kwenye Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.

makonda-2.jpg


RC Makonda alitoa ahadi kumsaidia Ahmed Albaity wakati wa Zoezi la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile Maumivu na Mateso anayopitia kijana huyo.

makonda-3.jpg


Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.

makonda-4.jpg


RC Makonda amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni zaidi ya Shilingi Million 100.

makonda-5.jpg


Aidha RC Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu, na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia na kufanikisha matibabu.

makonda-6.jpg


Hata hivyo RC Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Ahmed ili aweze kupona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

makonda-7.jpg

Kwa upande wa Ahmed Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

makonda-8.jpg

Aidha amesema alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona lakini RC Makonda ameonyesha moyo wa kipekee.



HONGERA MKUU WA MKOA MHESHIMIWA MR.MAKONDA KWA KUMSAIDIA MGONJWA KIJANA AHMED ALBAITY

chanzo.MAKONDA AFANIKISHA SAFARI NA MATIBABU YA AHMED ALBAITY CHINA - Global Publishers
 
Misuse of public funds.

Kwanini uyo asiombewe na KAKOBE au GWAJIMA Kuliko kutumia pesa zetu kwa issue ndogo hivyo.
Kakobe na Ngwajima ni wasanii wale wanawapanga watu wa kuwaombea sio wagonjwa wa ukweli. Kama ni kweli Kakobe na Ngwajima wanao uwezo wa kuwaombea Wagonjwa waende hospitali ya Muhimbili kuwaombea wagonjwa Wapo Wagonjwa Muhimbili wengi wanaohitaji kuombea Maomi mbona hawaendi akina Kakobe na Ngwajima?
 
Safi sana Makonda piga kazi usiwasikilize nyumbu
Mkuu wa mkoa Wa Dares-Salaam Mheshimiwa Mr Makonda mchapa kazi mzuri katika Serikali ya Mheshimiwa Mtumbuwa Majipu sugu Rais wetu Dr.Magufuli. Hongera Mr Maponda kwa kazi unazo zifanya ninakukubali sana.
 
Punda, behind ya ugonjwa wa huyo jamaa Kuna watu ni mapunda hapo by hundred percent!
 
Hizo gharama zote amegharamikia makonda au kuna mkono wa serikali??? Coz haingii akilini kwa mshahara wa mkuu wa mkoa ambao nna uhakika haufiki million hata nane kwa mwez aweze kutoa 100milion shillings on spot.... Hapo Kama nakosea ruhusa kunikosoa na kuniweka sawa
 
Hizo gharama zote amegharamikia makonda au kuna mkono wa serikali??? Coz haingii akilini kwa mshahara wa mkuu wa mkoa ambao nna uhakika haufiki million hata nane kwa mwez aweze kutoa 100milion shillings on spot.... Hapo Kama nakosea ruhusa kunikosoa na kuniweka sawa
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Mr Makonda hakutoa hizo pesa zote mfukoni mwake, alifanya Harambee kwa watu binafsi kachangisha mchango kwa watu wenye uwezo na yeye pia inaonyesha ametoa mchango wake. Ndio akaweza kufanikisha kumsafirisha huyo mgonjwa sikiliza video kwanza kabla ya kuuliza maswali acha uvivu wa kusikiliza video.
 
Hongera mheshimiwa Makonda,Mungu awe nawe na akulipe kwa kheri uliyoifanya,namuombea pia Ahmed Albaity Mungu amponye in sha Allah.
 
Nadhani wengine waende tu na wao watapewa huduma sawa sawa
 
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Mr Makonda hakutoa hizo pesa zote mfukoni mwake, alifanya Harambee kwa watu binafsi kachangisha mchango kwa watu wenye uwezo na yeye pia inaonyesha ametoa mchango wake. Ndio akaweza kufanikisha kumsafirisha huyo mgonjwa sikiliza video kwanza kabla ya kuuliza maswali acha uvivu wa kusikiliza video.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom