RC Makalla: Wananchi jitokezeni kupata Chanjo ya Uviko Wimbi la tano!

.kiiywa wanyonge mnakua wakali, lakini hayo yote mnayafanya sababu ya uonyonge wenu wa kupenda vya bure kwa jina la msaada
 
Mkoa wa Dar es salaam umezindua kampeni ya chanjo ya Uviko wimbi la tano ambapo wananchi wanaombwa kujitokeza na kupata chanjo ya ugonjwa huu hatari duniani.

RC Makalla amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote kwani ugonjwa huu sasa umeingia Wimbi la tano na ni hatari.

=====

RC MAKALLA: AWAHAMASISHA WANANCHI KUCHANGAMKIA CHANJO

-Apongeza MDH kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika mambo mbalimbali ya Afya na hasa Mapambano ya Uviko-19

-Asema Wananchi wanahitaji kupatiwa maarifa na kuelimishwa Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19

-Asisitiza Mdau Mkubwa wa Afya yako ni wewe mwenyewe hivyo Ujanja ni Kuchanja

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ameyasema hayo leo wakati anaongea na Wataalam wa Afya kutoka MDH na Sekretarieti ya Mkoa na Wilaya katika kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni ya kuongeza kasi ya kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa DSM kuchanja chanjo ya Uviko-19.

Kikao hicho kilimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Posta Ilala-Dar es Salaam.

RC Makalla amewapongeza MDH ( Management Development of Health) kwa kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali za Afya huku akibainisha MDH ni "partiner" mzuri wa Serikali.

"Ninauzoefu na NGO'S nyingi utakuta zina malengo mazuri na mikakati mingi lakini hakuna kinachofanyika niwapongeze sana MDH" Alisema RC Makalla

Aidha RC Makalla amesema wananchi katika makundi mbalimbali, popote walipo wahamasishwe na kupatiwa maarifa ya Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19 ili wawe na uelewa waweze kuchanja kwa hiari yao.

Hata hivyo RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya kupata chanjo na kuleta Chanjo za kutosha ambazo zimesaidia nchi yetu kuto kutengwa na kuwa sehemu ya Dunia kwa kuwa ilikuwa vigumu mtu kusafiri bila kuchanjwa.

Sambamba na hilo RC Makalla amebainisha mdau namba moja wa Afya yako ni wewe mwenyewe hivyo Ujanja ni Kuchanja, Chanjo ya Uviko-19 ni Salaam imethibitishwa na Wataalam wa Afya

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume amesema hali ya uchanjaji kwa Mkoa sio mbaya sana kinachotakiwa ni kuendeleza kasi ya Uhamasishaji na uelimishaji wa jamii juu ya Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19.

Kikao hicho kiliwajumuisha Viongozi wa Amani (Dini) Mkoa wa DSM, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wataalam kutoka MDH, Wilaya, na Sekretarieti ya Mkoa.
Hawa jamaa sijui vipi,nchi za Magharibi wala hazitaji uviko tena,na wanaondoa all mandates,yeye bado ana piga kelele watu wachanje!Kweli usichojua ni usiku wa giza.Swala la Uviko limeshatimiza malengo ya kuleta kwake,sasa tunasubiri matokeo.Pole pooole wanaufuta Uviko kwa kutumia Vita ya Ukraine,jamani mbona hii iko wazi?Are we really so dumb,tuamke.
 
Zoezi la watu kuchanja kwa hiari chanjo ya UVIKO 19 limedorora ile mbaya hapa nchini. Serikali ikitaka kufanikiwa, na kulipa zoezi hili uhai na hamasa mpya basi waipigie "promo" ya nguvu na waihusishe chanjo hii na suala la kuchochea "libido" tu.

Watafute na mashuhuda kadhaa wa uongo. Hapo ni lazima kizuri kitajitembeza chenyewe tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Huyu atasababisha tupigwe ban bureee,
Wakati watu wameshaanza harakati za kusafiri tena,
Mzee baba njoo huku wamachinga, bodaboda, malori bado ni usumbufu wa kutosha kabisa
HUYU MHESHIMIWA HAFIKIRII KWAMBA KUTOKANA NA HIYO KAULI YAKE ANAWEZA KUSABABISHA HAWA WATALII WACHACHE WANAOKUJA TUKAWAKOSA KABISA.
JUZI TU KENYA WAMETANGAZA KUONDOA ULAZIMA WA KUVAA BARAKOA HALAFU SISI TUNATAKA TENA KURUDI HUKO.
 
Hapa nilipo kuna NGO moja (jina kapuni) wametoa bonasi kwa watumishi wa afya ukipata mteja ukamshauri na akakubali kuchanja Uviko unapewa buku (sh. 1000 za kitanzania) kama unavyojua watanzania kwenye figisu huwa haturembi, nesi mmoja kwa siku anachanja watu 100, amewapata wapi wakati Kijiji kizima hatufiki 2000 na kila siku nesi watatu waliopo hapa wanalaza hesabu ya 100+ kila mmoja!
Wazungu oyeeee!
 
Nj
HUYU MHESHIMIWA HAFIKIRII KWAMBA KUTOKANA NA HIYO KAULI YAKE ANAWEZA KUSABABISHA HAWA WATALII WACHACHE WANAOKUJA TUKAWAKOSA KABISA.
JUZI TU KENYA WAMETANGAZA KUONDOA ULAZIMA WA KUVAA BARAKOA HALAFU SISI TUNATAKA TENA KURUDI HUKO.
Njaa mkuu, mkuu wa Mkoa anawapigia pande hiyo NGO ambayo inapiga hela za beberu!
 
Yule aliekuwa mkuu wa mkoa wa Dar ambaye sasa ni tapeli wa viwanja Dar aliwahi kufanya famigation ya mchongo katika jiji ila baba yake akamgundua
 
Tuko vitani SASA hivi.......chanjo na mabomu Bora ukwepe nini Kwanza ??😡😡😡
 
Chanjeni nyie wabongo ili msituletee variant mpya. Bongo ikifumua aina mpya ya korona, mtapigwa marufuku dunia nzima. Hata mabwana zenu Wachina watawakataza kuingia kwao.
 
Tulishapata pesa zao tukajengea madarasa, sasa hivi hawatoi tena wanazipeleka Ukraine...
 
Back
Top Bottom