RC Makalla, nunueni magari ya kufagia barabara; himizeni mama lishe kutumiia maji tiririka

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,389
4,054
Hivi sasa barabara zetu za Dar es Salaam zina lami pamoja na Mifereji. Lakini naona michanga barabara ni mingi na wafagizi wengi wanamwagia huo mchanga kwenye hiyo mifereji.

Hivyo ni vizuri mkanunua magari ya kufagia barabara na pili hiyo mitaro isafishwe. Maana la stand ya Mbezi na machinga ni gumu kwa sasa linahitaji ushirikishwaji zaidi.

Jingine, la mama lishe Posta nk waambie kama hakuna maji tiririka wataoshaje vyombo hivyo; unawaondoa kwa kutumia njia hiyo. La sivyo, sahani n.k wawe wanaosha kwa maji tiririka.
 
Baada ya miaka 2,3 lami yote inafunikwa na mchanga....lami haionekani
Badaye wanakuja kujenga tena

Ova
Kuna watu wana sema ni juhudi za makusudi, ili wapate tenda za kusafisha hiyo mitaro
 
Kuna watu wana sema ni juhudi za makusudi, ili wapate tenda za kusafisha hiyo mitaro
Miaka ya 70,80 sehemu nyingi kinondoni mjini kulikuwa na lami na taa mitaani
Ukiangali baadhi ya maeneo utaona kingo na chini lami imefukiwa na mchanga
Enzi za mzungu bryson
Naona bado sahvi tunarudi kule kule kuipoteza lami,sahv ukipita barabara nyingi sinza na kwengineko walipoweka lami mchanga upo
Na ktk kipindi cha miaka 2,3 barabara zote zitafunikwa na mchanga

Ova
 
Hii nchi ilishafeli since tulipomfukuza mkoloni. Hakuna wanachoweza zaidi ya kubaki madarakani.
 
Back
Top Bottom