RC Makalla hongera, umelisafisha Jiji la Dar

Machinga wameonewa tu,
Kero hasa kariakoo ni malori
Malori sasa hivi ni mtihani mkubwa sana
Na wanasema eti haya ni ya wakubwa
Ndio maana hawaguswi
So wacha wanyonge tusote tukisubiri magufuli mwingine
 
Kweli Jiji la Dar lazima lazima lipewe mtoto wa mjini kuliendesha.
Kwa mtaji wa tamko la Rais Samia, RC Amos Makalla amelisafisha Jiji la Dar tena bila vurugu za kupigana virungu.

Kwa mtu anayejua kuongoza mass dwellings , ni lazima hatua ya kuondoa machinga imekuwa very well planned.

RC Makalla nakupa pongezi kwa hilo.

Machinga lilikuwa janga la afya
Machinga ilisababisha ajali barabarani
Machinga na vibanda ilikuwa maficho ya vibaka
Machinga hawalipi kodi.
Machinga waliziba mitaro ya usafi wa maji ya mvua.

Sasa Jiji la Dar linarudi kwenye ubora wake.

Hongera sana Amos.
Mkuu hapo ni sawa ila bado malori
Haya malori kariakoo ni shida kuliko hata wamachinga na nasikia ni ya wakubwa so ofisi za usafirishaji zimejaa kariakoo na kuziba barabara hadi kero
Hawaguswi hawa tunaonewa wamachinga tu?
Hembu lisemee na hili
 
RC Makala hakika anastahili pongezi kubwa na timu yake.

Sasa shughulikia mgogoro wa ardhi kule Mbopo haki itendeke kwa wenye maeneo yao kurejeshwa kwa wamiliki halali wa awali.
 
Nimemshangaa sana Rev. Gwajima juzi anajifanya kutetea wahalifu wavamizi wa maeneo ya watu ,

Yani Gwajima una furahia uhuni wa wavamizi kupora maeneo ya watu kihuni?

Wewe wangevania eneo lako ungejisikiaje?

Unatetea uhalifu ?

Tutajenga jamii ya aina gani?

Wenye maeneo halali wana mikopo mikubwa wanarejesha kila mwezi na wengine ni wastaafu halafu unatetea wavamizi wa maeneo ya watu Gwajima?

Yani juzi ulinishangaza sana!
 
Back
Top Bottom