#COVID19 RC Makalla: Daladala Dar es Salaam zibebe abiria level seat wanafunzi watano watasimama na wote wavae barakoa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,613
141,436
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameviagiza vyombo vya usalama kuhakikisha daladala zinabeba abiria level seat na kwamba wanaoruhusiwa kusimama ni wanafunzi wasiozidi watano.

Wanafunzi watasimama katika umbali wa mita moja kutoka mmoja hadi mwingine na wote wavae barakoa.

Kadhalika abiria wengine wote lazima wavae barakoa.

Chanzo: ITV habari!
 
Level seat iwe buku buku nauli😎 na wazingatie AC iwashwe sio kulipa buku vioo wazi na gari ipite kwenye mwendokasi road! Ili watu wawahi kufika makwao na hizo level seat zao!
 
Hili la Daladala hasa za Dar es Salaam kutopakia 'Nyomi' na kuanza Kupakia 'Level Seat' kwa hali ya Usafiri ilivyo Ngumu likifanikiwa naahidi Kutembea kwa Miguu tena 'Pekupeku' kutoka hapa Mkoani Dar es Salaam ( Mzizima ) hadi Kwetu Mkoani Mara ( Musoma )
 
Huyu nae hivi hajajishtukia tu kama watu wamemdharau?
Nashangaaa!!tangu atoe tamko wananchi wana mcheki tu, eti wanafunzi ndio wasimame kwa umbali wa mita moja moja, sasa kwenye daladala c watasimama kama watatu tu!!!?waache watu waendelee na maisha yao tu, kwani siasa zao ndio zinawavuluga wananchi!!
 
Wengine wanaonaga upumbafu ni fasheni dar ina bahati mbaya aliondoka mwenye mkoa wake kaja tena kiherehere mwingine
 
Back
Top Bottom