RC Makalla aagiza Polisi kuanza operesheni ya kukamata wezi wa vifaa vya magari na vibaka Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Ni Kufuatia Wizi huo kuibuka upya kwenye baadhi ya maeneo.

- Vibaka wanaosumbua mtaani kukiona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.

IMG-20210927-WA0012.jpg
IMG-20210927-WA0018.jpg
 
Aangalie asije akajikuta kwenye ufuatiliaji huo ikaonekana gari lake limefungwa spea kutoka Gerezani, Kamata, Machinga complex, Buguruni, Ilala, Temeke, Tandika.

Makonda alifanyza zoezi hilo mwanzoni kwa ufanisi lakini mwishoni likageuka kaa la moto na soko hilo likarejea kwa kasi na nguvu sana hadi leo polisi wanapita tu bila kuwabughudhi
 
Aanze na gerezani, wale wauzaji wa vifaa vya uwizi wa magari watataja wezi wote hapa mjini. Kamateni pale gerezani wauza vifaa vya uwizi, polisi wanawajua sanaaa
Wauzaji na wafadhili wenyewe ndio hao hao wakamataji. Ni nani kwenye jiji hili asiyejua vifaa vya magari vya wizi vinapatikana wapi? Sio yeye tu Makala, IGP alishatoa tamko na baadhi ya vifaa vilikamatwa vikalazwa vingi tu pale Central pamoja na Noah mbili, ulisikia muendelezo wa ile kesi? Wahusika walikamatwa? Walifikishwa mahakamani? Mahakama iliwatia hatiani?

Wizi wa vifaa vya magari, pesa ndefu kwenye mabenki na taasisi, biashara ya dawa za kulevya, ujangili, ukwepaji kodi mkubwa, wizi qa mali za umma, n.k haya yote ni mzizi wa ustawi wa chama na wanachama na chama kina wenyewe.
 
Upuuzi tu. Sirro alishaagizwa na bosi wake Rais kuhusu hili. Anataka kusema kuwa Sirro alidharau agizo la bosi wake yaanu mkuu wa nchi!?
 
Ni Kufuatia Wizi huo kuibuka upya kwenye baadhi ya maeneo.

- Vibaka wanaosumbua mtaani kukiona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.
View attachment 1954803View attachment 1954804View attachment 1954805View attachment 1954806View attachment 1954807View attachment 1954809
Dah hii habari njema sana tena sana, tumeteswa sana na hawa wezi wa vifaa vya magari
 
Ni Kufuatia Wizi huo kuibuka upya kwenye baadhi ya maeneo.

- Vibaka wanaosumbua mtaani kukiona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla
ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.

Yeye mwenyewe ni kibaka pamoja na hao polisi wake
 
Dah hii habari njema sana tena sana, tumeteswa sana na hawa wezi wa vifaa vya magari

Inamaana bila tamko la mkuu wa mkoa tungeendelea kuhenyeshwa? Kwamba polisi hawajui na hawaoni kabisa tunavyoibiwa vifaa vya nagari mtaani?
 
Makonda alikua na matamko mengi, na anayaanza lakini hayamalizi.

Huyu ana matamko mengi zaidi ambayo hayatekelezwi na hao anaowaagiza. Anaibua hili kabla halijaanza anapachika jingine, matokeo yake tunazoea tu kuona " makala kaagiza hiki mala kile""
 
Si lazima aongee ili ajulikane ana akili timamu.
Kwani kabla ya kauli hii vibaka walirusiwa dar?
Awainue wajasiriamali kama ana akili.
 
Makala tamko lako la kuvaa barakoa, level seat na kuchanja yote yamepuuzwa na wasaidizi wako.

Chanjo zimeshaanza ku-expire.
 
Back
Top Bottom