RC Makala: Rais Samia ametoa Tsh 100 milioni kuboresha soko la Machinga Complex, kutazungushwa bati na meza za kisasa

Rais Samia ametoa tsh milioni 100 ili kuboresha soko la Machinga comllex na kuwezesha wamacbinga wote wa kariakoo kuhamia hapo Karume

RC Makalla amesema maboresho yanaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio wa mabati na kuweka meza za kisasa za kupanga biashara

Chanzo: ITV habari
Hilo nalo ukalichome moto
 
uzio wa mabati na meza za kisasa 100M?

Machinga complex wafanyabiashara hawapataki wateja wakibongo wanatabia ya uvivu hawatapanda lile gorofa...
Yani hii concept serikali imeshindwa kabisa kuelewa, mmachinga hatembei barabarani kisa hana sehemu ya biashara, anakaa barabarani ambapo watu wanapita kutafuta wateja.

Wewe unataka kumpeleka floor ya nne huko na kumpatia chumba cha biashara, hapa ndo utajua kuwa tunaongozwa na watu wasiojua uhalisia wa maisha
 
Rais Samia ametoa tsh milioni 100 ili kuboresha soko la Machinga comllex na kuwezesha wamacbinga wote wa kariakoo kuhamia hapo Karume

RC Makalla amesema maboresho yanaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio wa mabati na kuweka meza za kisasa za kupanga biashara

Chanzo: ITV habari
Huu UJINGA wa Rais ametoa utaisha lini?
 
Yani hii concept serikali imeshindwa kabisa kuelewa, mmachinga hatembei barabarani kisa hana sehemu ya biashara, anakaa barabarani ambapo watu wanapita kutafuta wateja.

Wewe unataka kumpeleka floor ya nne huko na kumpatia chumba cha biashara, hapa ndo utajua kuwa tunaongozwa na watu wasiojua uhalisia wa maisha
Pale wakarabati tu ila watu hawaendi. halafu hata ruti yake imekaa vibaya mtu apande mwendokasi ashukie gerezani achukue boda??
 
Rais Samia ametoa tsh milioni 100 ili kuboresha soko la Machinga comllex na kuwezesha wamacbinga wote wa kariakoo kuhamia hapo Karume

RC Makalla amesema maboresho yanaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio wa mabati na kuweka meza za kisasa za kupanga biashara

Chanzo: ITV habari
Hivi wakisema Serikali imetoa watapungukiwa nini? Samia hizo hela anatoa kwa utashi wake au anatoa mfukoni kwake?

Mwendazake walimpamba namna hii hadi kaburini. Haikusaidia kitu
 
uzio wa mabati na meza za kisasa 100M?

Machinga complex wafanyabiashara hawapataki wateja wakibongo wanatabia ya uvivu hawatapanda lile gorofa.

walishapewa vizimba wakavikimbia.

Kibongobongo mfanyabiashara anamfuata mteja na sio mteja kumfuata mfanyabiashara. Ndio maana mabiashara yamejaa barabarani
Wauze bei za machinga watapata wateja wasiuze kama bei za kinondoni
 
Ubaya wa Machinga Coplex huko gorofani utakuwa unauza nini ambacho pale ground floor hakipo??

Kule gorofani wamejaa mafundi wa laptops/sim na hao wapo 2nd floor
 
Rais Samia ametoa tsh milioni 100 ili kuboresha soko la Machinga comllex na kuwezesha wamacbinga wote wa kariakoo kuhamia hapo Karume

RC Makalla amesema maboresho yanaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio wa mabati na kuweka meza za kisasa za kupanga biashara

Chanzo: ITV habari
Mambo ya kipuuzi kabisa haya.
Hivi vyeo vya 'ukuu ukuu' vifutwe tu.
Katiba mpya itawafunza adabu hawa mchwa.
 
Rais Samia ametoa tsh milioni 100 ili kuboresha soko la Machinga comllex na kuwezesha wamacbinga wote wa kariakoo kuhamia hapo Karume

RC Makalla amesema maboresho yanaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio wa mabati na kuweka meza za kisasa za kupanga biashara

Chanzo: ITV habari
Huu ndio ujinga..tulio ukataa hizo hela kazitoa kwenye mkoba wake..au hela za watanzania za walipa kodi..wanasiasa wasipo acha upuuzi huu wakujiona ndio wamiliki wa nchi ipo siku..watadharirika.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nawaona Machinga wakifukuzwa KKOO ndani ya siku 30 zijazo
Mkuu Root sio wanafukuzwa bali wanapelekwa mahali salama kwa biashara zao. Tambua kuwa wamachinga ni wale wanaotembeza biashara zao, hawa hawahitaji eneo la kufanyia kazi.

Hawa wa Soko la Kariakoo sio WAMACHINGA ni WAJASILIAMALI wanao hitaji eneo salama la kufanyia biashara zao, ambalo watalipia kodi ya leseni na kodi ya pango.

Aidha mtaji wao ni mkubwa na wengine huwazidi hata wafanyabiara waliopanga kwenye maduka ya biashara ambao wanalipa pango na leseni. Kutokana na udhaifu na mapungufu ya Serikali Wajasiliamali hawa wamesoma gepu na kujiita wao ni WAMACHINGA jambo ambalo si kweli.

Serikali ifuate sheria, taratibu na kanuni za biashara, sio kila eneo ni la biashara. Uholela huu wa biashara kwa asilimia kubwa ni uoga wa watawala kwenye KURA ZA HAWA WAJISILIAMALI waliojificha mgongoni mwa WAMACHINGA.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom