RC Makala leo 31/8/ yupo Kibamba kusikiliza kero za wananchi.

Ziara za saivi ni porojo tupu na kujilipa posho. Hakuna maamuzi yoyote.

Bora wabaki tu ofisini tujue wananchi tunapambana je?
 
Wakuu watakao weza kuhudhuria wakazi wa Mpiji magoe wamuulize kuhusu barabara yetu toka mbezi eneo la Mbezi high - Mpiji hakika barabara ni mbovu haifai magari kila baada ya mwezi ni kubadili bush, tunahitaji lami kama JIWE alivyotuahidi.
 
BARABARA YA KUTOKA BAGAMOYO ROAD -MABWEPANDE NI MBOVU SANA
DARAJA LINALOUNGANISHA SHULE YA STAMARIA SALOME NA BOKO SEKONDARI LIMECHUKULIWA NA MAJI TANGU MWAKA 2013 HADI LEO HAKUNA JUHUDI ZA KULIJENGA UPYA WANANCHI NA WANAFUNZI WANATESEKA SANA MSIMU WA MVUA
 
siku moja nimeenda kituo cha Polisi Cha wilaya ya Ubungo kilichopo Kiluvya gogoni, kinapaswa kiboreshwe kwani kinahudumia eneo kubwa la wilaya nzima ya Ubungo.
hakuna Daladala zinazo fika mpaka kituoni hapo, daladala nyingi zinaishia kibamba hivyo kuna haja ya kujenga kituo kikubwa cha daladala ktk maeneo hayo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanao fuata huduma ktk kituo hicho cha Polisi ambacho ndio kinahudumia wilaya nzima ya Ubungo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom