jembelamkono
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 2,733
- 2,011
Akiwa kama mkuu wa mkoa wa Mara,leo hii ameitoa kauli hiyo wilayani Nyamongo ambapo ameviasa vyombo vya dola kudeal na makundi ya wahuni kihuni hivyo hivyo.
Hii ni baada ya kundi la wanakijiji walivamia kituo cha afya na kuharibu mali baada ya raia mmoja kupigwa risasi.
My take;
Je kauli hii imekaaje hasa ukizingatia kama kiongozi katika mkoa anatakiwa kuongoza kwa kuzingatia utawala wa sheria?

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Mara mh. Magesa Mulongo jana mimi binafsi kupitia taarifa ya habari aliniacha na butwaa baada ya kuagiza jeshi la polisi mkoani mara kuwashughulikia mara moja wote waliohusika katika vurugu kati ya jeshi la polisi na wananchi katika hospital mkoani humo kufuatia wananchi kupinga mauaji yanayoendelea katika migodi mkoani humo.
Mulongo aliwaambia jeshi la polisi kwamba hawa ni wahuni wanaojificha katika mgongo wa kudai haki hivyo washughulikiwe na ikiwezekana hakuna haja ya kuwafikisha wanapostahili kufika. Binafsi sentensi hiyo ya mwisho ndiyo iliyinipa tabu. Labda mimi sikumwelewa au nilimwelewa kupita kiasi. Si lugha lugha ya kariba ya kiongozi wa aina ya mkuu wa mkoa.
Ifike wakati hawa wakuu wa mikoa wabadilike na wafuate misingi ya utoaji haki.