RC Kunenge na Waziri Ummy Mwalimu, dhibitini suala la uchafu katika jiji la Dar es Salaam

was njombe

Member
Sep 8, 2020
6
45
Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam nakupa hongera kwa nafasi uliyopewa. Mh Rais amekuamini na mimi nakuamini. Miundombinu kama inavyoimarishwa kwa kweli Serikali hii itakumbukwa kwani nia na madhumuni jiji hili lifanane km majiji mengine duniani.

Lakini naomba sana pamoja na Serikali kwa ujumla wake hapa naomba sana Waziri wa Mazingira Mh. Ummy Mwalimu unisikie. Jiji la Dar es Salaam ni chafu Sana na uharibifu wa Mazingira na sasa imekuwa ni tabia ya wakazi kuishi na uchafu.

Mh. Kunenge angalia ninakuonesha bustani za barabara wamachinga wameharibu; yaani barabara zote zenye bustani na mandhari ya mji zimegeuka kuwa dampo na njia za mkato.

Barabara hizi ni kodi zetu na Sheria tunazo lakini tumekwama wapi hata tushidwe kuzitumia? Angalia stendi ya daladala Mbezi Louis kila asubuhi mapema ukifika aibu, mitaro na eneo lote linalozunguka uchafu usio elezeka. Kimara darajan hakufai. Pokea sehem ya ushauri ninaokupa moja.

TANROAD mkoa wa Dar waingie barabarani kuweka zuio. Pili Serikali za mitaa wenyeviti Kama eneo lake lenye haraiki ni chafu basi na yeye ni mchafu afukuzwe kazi.

Asante. Tunaomba namba yako kwa mawasiliano kwa umma ijulikane.

Kwako Mh. Kunenge na Ummy Mwalimu
 
Teenager

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
1,432
2,000
Uchafu mara nyingi unatokana na umasikini unaopelekea kukosa ustaarabu.

Pia uchafu sio barabarani tu bali mitaani.

Na mitaani ndipo wanapoishi wananchi hivyo kunamatter zaidi.

Nashauri jiji zima la dar hasa mitaani waanze kuzipangilia nyumba upya zimebanana na kukaa hovyo sana hiyo inachangia uchafu.

Pia waanze kujenga mifumo mizuri ya maji taka mitaani na barabarani yani sewers.

Pia waweke viwango vya nyumba zinazotakiwa kujengwa.

Pia waanze kujenga urban parks ili watu wapate kupumzika jioni au weekend na kupunga hewa safi na kuosha macho kwa ukijani sio vumbi tu kila sehemu.

Na waanzishe mradi wa kupanda miti na nyasi dar na mitaa yake yote hiyo itaondoa vumbi dar nzima.

Waondoe machinga na wafanya biashara wadogo mitaani na mabarabarani na kuwajengea masoko yao maalum ya kufanyia biashara na ni lazima usafi uwe wa kiwango cha juu or wawajengee malls zao.

Ukiachana na malls za machinga pia watengeneze malls kubwa za viwango vya juu ili kuvutia wafanya biashara kutoka nje pia sisi wenyewe hiyo itakuza uchumi kwa kasi ya mwendo kasi.

Wajenge sehemu maalum za kuchoma taka za aina zote.

Pia waje na kampeni za kunua mapipa maalum na mifuko maalum ya taka.

Na wanunue magari maalum ya kuzoa taka yanayotumia machine na hiyo iwe sekta kabisa ya kutoa ajira kwa madereva.

Wajenge au kupitisha barabara nzuri zinazopita mitaani katikati ya mistari ya nyumba zoote baada ya kupangwa.

Kila mtu awe anatozwa kodi ya usafi hiyo itakuwa ajira na sekta maalum za usafi Tanzania nzima.

Na kila atakayejaribu kukiuka sheria za usafi basi apigwe faini.

Hayo yote bajeti yake na effort inayotakiwa ni kubwa lakini effect na faida yake ni kubwa mno.

And i think baada ya 5 years dar itakuwa zaidi ya new York au dubai pamoja na London.

Kama dar au Tanzania nzima ikiwa hivyo basi kila mtu na wawekezaji pia watalii na wafanya biashara watavutika kuja Tanzania hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na lazima ajira ziongezeke.

Hapo tutegemee African Americans na watu duniani kote kuzamia Tanzania.

Hivi walikuwepo wapi muda wote kwanini hawakufanya hivi vitu 20 years ago?
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,960
2,000
Kila mtu ana umuhimu wake...kwa mbaaali watu wameanza kumkumbuka Mh. Makonda, jiji lilipendeza angalau! Kuna siku hizi kelele za "chato" tutazijutia!
 
Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,754
2,000
Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam nakupa hongera kwa nafasi uliyopewa. Mh Rais amekuamini na mimi nakuamini. Miundombinu kama inavyoimarishwa kwa kweli Serikali hii itakumbukwa kwani nia na madhumuni jiji hili lifanane km majiji mengine duniani.

Lakini naomba sana pamoja na Serikali kwa ujumla wake hapa naomba sana Waziri wa Mazingira Mh. Ummy Mwalimu unisikie. Jiji la Dar es Salaam ni chafu Sana na uharibifu wa Mazingira na sasa imekuwa ni tabia ya wakazi kuishi na uchafu.

Mh. Kunenge angalia ninakuonesha bustani za barabara wamachinga wameharibu; yaani barabara zote zenye bustani na mandhari ya mji zimegeuka kuwa dampo na njia za mkato.

Barabara hizi ni kodi zetu na Sheria tunazo lakini tumekwama wapi hata tushidwe kuzitumia? Angalia stendi ya daladala Mbezi Louis kila asubuhi mapema ukifika aibu, mitaro na eneo lote linalozunguka uchafu usio elezeka. Kimara darajan hakufai. Pokea sehem ya ushauri ninaokupa moja.

TANROAD mkoa wa Dar waingie barabarani kuweka zuio. Pili Serikali za mitaa wenyeviti Kama eneo lake lenye haraiki ni chafu basi na yeye ni mchafu afukuzwe kazi.

Asante. Tunaomba namba yako kwa mawasiliano kwa umma ijulikane.

Kwako Mh. Kunenge na Ummy Mwalimu
Na RC ambaye mkoa wake ni mchafu naye atakuwa mchafu, afukuzwe kazi
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,944
2,000
Soko la Kawe kuna uchafu wa mitaro hatari kubwa sana.

Soko la samaki wa kukaanga nzi wanaruka toka mtaroni wanatua kwenye kitoweo (samaki ) ni zaidi ya hatari.

Halafu pale ni karibu na chooni jamani!

Mitaro ya maji machafu sokoni hata pale soko la kuku la mwenge parekebisheni.

Mtu ni afya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom