RC Kunenge amtaka Mkandarasi wa Barabara ya Mwinyijuma Mwananyamala kuikabidhi ifikapo 30 Juni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,761
141,627
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Kunenge amekagua ujenzi wa barabara ya Mwinyijuma Mwananyamala na kusikitishwa na kusuasua kwa ujenzi huo.

Kunenge ameagiza Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana na ahakikishe amekabidhi barabara hiyo ifikapo 30/6/2021 ikiwa imekamilika vinginevyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mzee Mgaya ambaye ni mwenyeji wa CCM Mwinyijuma ameshukuru kwa ziara hiyo ya mkuu wa mkoa.

Chanzo: Upendo TV

Maendeleo hayana vyama!
 
Huwa nashangaa sana. Hivi mkandarasi anapojenga barabara haingii mkataba? Bilka shaka jibu ni ndiyo. Huwa anaingia mkataba na nani? Huwa ni nani anawajibika kusimamia ili ujenzi uende kama ilivyowekwa kwenye mkataba?

Kama kuna msimamizi kwa nini kazi inaposua sua asitekeleze wajibu wake mpaka angojee msukomo wa mkuu wa mkoa? Na mkuu wa mkoa kwanini asimwajibishe msimamizi? Au nimekosea na utaratibu ni kuwa mkuu wa mkoa ndiye msimamizi mkuu?
 
Kunenge ameagiza Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana na ahakikishe amekabidhi barabara hiyo ifikapo 30/6/2021 ikiwa imekamilika vinginevyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mzee Mgaya ambaye ni mwenyeji wa CCM Mwinyijuma ameshukuru kwa ziara hiyo ya mkuu wa mkoa.
Kwa vitisho tu hatujambo, vitisho tangu enzi na enzi lakini matokeo 0
 
Huwa nashangaa sana. Hivi mkandarasi anapojenga barabara haingii mkataba? Bilka shaka jibu ni ndiyo. Huwa anaingia mkataba na nani? Huwa ni nani anawajibika kusimamia ili ujenzi uende kama ilivyowekwa kwenye mkataba?

Kama kuna msimamizi kwa nini kazi inaposua sua asitekeleze wajibu wake mpaka angojee msukomo wa mkuu wa mkoa? Na mkuu wa mkoa kwanini asimwajibishe msimamizi? Au nimekosea na utaratibu ni kuwa mkuu wa mkoa ndiye msimamizi mkuu?
Haya mambo vurugu tupu...miradi kuna contract na contract kati ya client na contractor na msimamizi ( Consultant..sasa mie huwa nashindwa kuelewa, unless vinginevyo, consultant huwa anatoa montly progress work report kwa Client, inayotakiwa kueleza progress, changamoto, malipo yaliyofanyika, matatizo nk.hii yote kupata picha ya miradi unavyokwenda. Miradi mingi kawaida inakuwa guided na Conditions of Contract zinazospecify, kitu gani kitafanyika incase either party, atadefault. Kama ni delays kutokana Client au contractor, conditions of contract itasema nini kifanyike and so on. Sasa mie nashindwa kuelewa shida inakuwa wapi hadi RC aje kutoa site instructions , yaani consultant hakuwa anatoa montly work progress reports au vp. Kumbuka kama kuna delays due to weather or contractor delays, conditions of contract, inaelekeza what to do. Sasa mambo haya mengine naona sijui vp. Lazima kuna tatizo mahali.
 
10% inatafutwa tu hapo hakuna la maana

Asante sana kwa maelezo mazuri. Kweli kama mambo ndiyo yako hivyo hii RC kuibuka na maagizo inaonyesha kuna kitu hakiko sawa
 
Unafahamu kwa akina Chiku Kambi pale karibu na kwa akina rip Joseph Katuba kipa wa zamani wa Simba yaani nyuma ya nyumba ya mzee Bamaga?
Ule mtaa kuelekea wami bar zamani
Zamani pia bamaga ndy alipoanzia kufanya biashara ya mafuta....
Basi nshamjuaa mwambie mzee mgaya kna siku kna bahari mhuni wa zamani atakuja mtembelea

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hii haikubaliki kabisa yaani toka pale kona ya mwananyamala mpaka makumbusho miezi yote hiyo??

Anajua anasababisha usumbufu wa namna gani kwa watumiaji wa hiyo Barabara ??

Mbona Mkuu wa mkoa kaamua kulea hilo jipu ??

Sasa kwa spidi hiyo angepewa kujenga barabara yenye urefu mkubwa si angechukua miaka kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom