Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Za asubuhi wakuu hapa JF.Tunaendelea kuomboleza,Mungu tusaidie.
Mh Said Meck Sadick ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkoa wa kwanza Tanzania kwa kuwa na wasomi , wafanyabiadhara, watalii wengi na maendeleo yake kwa ujumla. Kifupi n Mkoa maarufu huko duniani kutokana na vitega uchumi vyake na mali asili zilizopo ndani ya Mkoa.
RC huyu kwakweli ni mtu wa kusikiliza, kujali na kutoa nafasi kwa utaalam fulani katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo. Ni kiongozi mchapakazi, msikivu, anajali wananchi wanyonge lakini pia anajua shida za wananchi wake hata wale wa vijijini. Ni mtu anayefuata wananchi hukohuko waliko.Hajikwezi.
Miaka ya nyuma, Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa na migogoro mingi sana ya ardhi na mipaka hasa maeneo yanayopakana na Mikoa ya Arusha na Manyara. Kwa uwepo wake, dawa imeshapatikana. Ni mtu ambaye anasikiliza sana wataalam huwa wanasema nini, wanashauri nini, kipi wanakikataa na kipi wanakikubali (kwa sababu za kitaalam).
Akiambiwa hapa maji hayapandi,anaelewa. Akiambiwa eneo hili ni la mwekezaji kisheria na nyaraka zipo, anaelewa (baada ya kuzizibitisha kisheria).
Mh Neck Sadick hata akienda kutembelea mradi unaojengwa sehemu fulani, huwa anaanza kwanza kwa kusikiliza pande zote yaani Mkandarasi, Consultant, Msimamizi kwa upande wa serikali nk ,hata kama kuna wanafiki wamepeleka umbeya ofisini. Ni mtu mwelevu sana. Hana papara,anashaurika na kutekeleza ushauri.
Sasa hivi Mkoa wa Kilimanjaro kimyaa, tuli kama maji ya mtungi. Hata kipindi kile yupo Dsm, mambo hayakuwa hovyo kama ilivyo sasa. Hakimbizi wananchi, hakimbizi wafanyabiashara, hana kinyongo nao. Waandishi wa habari ni watu wake wa kazi.
MaRC wengine (hasa vijana) wanaweza kujifunza mbinu za kiuongozi toka kwa huyu RC wa Kilimanjaro.Rais hakukosea kabisa.
Hongera sana RC Kilimanjaro, hongera nyingi Mh Rais kwa uteuzi uliotukuka wa huyu kiongozi safi asiye na kinyongo na wananchi , wafanyabiashara na wataalam/watumishi ndani ya Mkoa wake.
Tumsifu Yesu Kristo.