RC Kilimanjaro, Anna Mghwira: Nzige walionekana Moshi na kisha kupotea. Haijathibitika hasa walipo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,291
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amethibitisha nzige kuonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 wilayani Moshi na kupotea ila bado hawajathibitisha eneo walipo

Taarifa zaidi zinakuja.....
=====

Taarifa zaidi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema kundi la nzige limeonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 Wilaya ya Moshi na kisha kutokomea kusikojulikana, kwamba hadi leo Jumatatu Februari 10, 2020 hawajathibitisha walipo.

Ameeleza hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa za nzige hao kuingia Tanzania kutoka nchi jirani ya Kenya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema juzi walipata taarifa kuwa nzige hao wapo kilometa 50 kufika Wilaya ya Mwanga lakini walifuatilia kwa watu wa Taveta nchini Kenya na kupata taarifa kuwa bado hawajafika, lakini jana jioni walionekana Wilaya ya Moshi na kupotea.

"Tulifuatilia Taveta lakini wao walituambia hawajafika kwao, hivyo tukajiridhisha hata kwetu hawajafika kwa kuwa hawajapita Taveta lakini jioni walionekana Moshi na kupotea" amesema.

Amebainisha kuwa kwa sasa wataalamu wako maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama kuna eneo ambalo nzige hao wameingia na taarifa itatolewa baada ya wataalamu hao kujiridhisha.

Amesema kwa sasa vipepeo ndiyo wameonekana wako wengi na tayari wamewasiliana na wataalamu nchini Kenya ambako pia wapo kwa wingi.

Januari 29, 2020 Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga alisema Serikali itatumia ndege za kukodi kukabiliana na nzige ikiwa wataingia nchini kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.

Ameeleza hayo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tishio la nzige nchini.

Amesema walioonekana wilayani Loliondo walikuwa panzi si nzige.

Amebainisha kuwa Serikali imeandaa lita 7,000 za viuatilifu vya kuua nzige hao kwa kutumia ndege ambazo watazikodi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na shirika la kimataifa la kukabiliana na nzige.

Aliwataka wananchi na wadau wa kilimo kutoa taarifa ikiwa watabaini viashiria vya nzige katika maeneo yao.
 
Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,499
2,000
Watakuwa walikatiza usangi wakakutana na mtego wa wapare wakaliwa woooote.
Au walipotea njia wakapita karibu na kwa yule mbunge mwenye nuksi anayejiita dokta ambaye alipendekeza Zitto auwawe wakalogwa wakafa wote
Alijiita dokta
 
Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,421
2,000
Kama ndege za kunyunyuzia dawa zitakodia, je ni kwanini serikali isichukue hatua ya kununua hizo ndege badala ya kununua mapangaboi?
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,031
2,000
Duu utafikiri ndege za jeshi zisionekana hata kwa radar
Mbona hata satellite zinaweza kuonyesha kwa wingi wao au hatuna urafiki tena na wazee wa dunia wakatuambia wako wapi
Yaani hao naona wapo mlimani wameona kuna upepo mkali wakaamua kubana kwanza

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,598
2,000
Hapo kuna mmojawapo hasa RC atakuwa alidanganywa kwamba kuna nzige wameshaingia mkoani mwake na yeye akaingia kichwa kichwa na kutangazia umma kwamba nzige wameshawasili. Baadae akaja kugundua kwamba haikuwa kweli na akajitokeza tena kutangaza kwamba wametoweka. Ni nzige gani hao waje kutalii kimya kimya wasionekane na kupigwa hata picha na pia waondoke kimya kimya bila kuwaachia kilio wananchi wenye mashamba kwa kula mazao yao? Au walikuja wakiwa tayari wameshashiba?
 
Jiwe la kudumu

JF-Expert Member
Aug 17, 2018
296
250
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amethibitisha nzige kuonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 wilayani Moshi na kupotea ila bado hawajathibitisha eneo walipo

Taarifa zaidi zinakuja.....
=====

Taarifa zaidi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema kundi la nzige limeonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 Wilaya ya Moshi na kisha kutokomea kusikojulikana, kwamba hadi leo Jumatatu Februari 10, 2020 hawajathibitisha walipo.

Ameeleza hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa za nzige hao kuingia Tanzania kutoka nchi jirani ya Kenya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema juzi walipata taarifa kuwa nzige hao wapo kilometa 50 kufika Wilaya ya Mwanga lakini walifuatilia kwa watu wa Taveta nchini Kenya na kupata taarifa kuwa bado hawajafika, lakini jana jioni walionekana Wilaya ya Moshi na kupotea.

"Tulifuatilia Taveta lakini wao walituambia hawajafika kwao, hivyo tukajiridhisha hata kwetu hawajafika kwa kuwa hawajapita Taveta lakini jioni walionekana Moshi na kupotea" amesema.

Amebainisha kuwa kwa sasa wataalamu wako maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama kuna eneo ambalo nzige hao wameingia na taarifa itatolewa baada ya wataalamu hao kujiridhisha.

Amesema kwa sasa vipepeo ndiyo wameonekana wako wengi na tayari wamewasiliana na wataalamu nchini Kenya ambako pia wapo kwa wingi.

Januari 29, 2020 Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga alisema Serikali itatumia ndege za kukodi kukabiliana na nzige ikiwa wataingia nchini kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.

Ameeleza hayo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tishio la nzige nchini.

Amesema walioonekana wilayani Loliondo walikuwa panzi si nzige.

Amebainisha kuwa Serikali imeandaa lita 7,000 za viuatilifu vya kuua nzige hao kwa kutumia ndege ambazo watazikodi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na shirika la kimataifa la kukabiliana na nzige.

Aliwataka wananchi na wadau wa kilimo kutoa taarifa ikiwa watabaini viashiria vya nzige katika maeneo yao.
Ana hamu ya kutumbuliwa kama Mwere
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
36,615
2,000
Watakuwa walikatiza usangi wakakutana na mtego wa wapare wakaliwa woooote.
Au walipotea njia wakapita karibu na kwa yule mbunge mwenye nuksi anayejiita dokta ambaye alipendekeza Zitto auwawe wakalogwa wakafa wote
🤣🤣🤣🤣🤣 waligeuzwa "Kijoooo"
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,500
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amethibitisha nzige kuonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 wilayani Moshi na kupotea ila bado hawajathibitisha eneo walipo

Taarifa zaidi zinakuja.....
=====

Taarifa zaidi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema kundi la nzige limeonekana jana Jumapili Februari 9, 2020 Wilaya ya Moshi na kisha kutokomea kusikojulikana, kwamba hadi leo Jumatatu Februari 10, 2020 hawajathibitisha walipo.

Ameeleza hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa za nzige hao kuingia Tanzania kutoka nchi jirani ya Kenya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema juzi walipata taarifa kuwa nzige hao wapo kilometa 50 kufika Wilaya ya Mwanga lakini walifuatilia kwa watu wa Taveta nchini Kenya na kupata taarifa kuwa bado hawajafika, lakini jana jioni walionekana Wilaya ya Moshi na kupotea.

"Tulifuatilia Taveta lakini wao walituambia hawajafika kwao, hivyo tukajiridhisha hata kwetu hawajafika kwa kuwa hawajapita Taveta lakini jioni walionekana Moshi na kupotea" amesema.

Amebainisha kuwa kwa sasa wataalamu wako maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro ili kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama kuna eneo ambalo nzige hao wameingia na taarifa itatolewa baada ya wataalamu hao kujiridhisha.

Amesema kwa sasa vipepeo ndiyo wameonekana wako wengi na tayari wamewasiliana na wataalamu nchini Kenya ambako pia wapo kwa wingi.

Januari 29, 2020 Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga alisema Serikali itatumia ndege za kukodi kukabiliana na nzige ikiwa wataingia nchini kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.

Ameeleza hayo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tishio la nzige nchini.

Amesema walioonekana wilayani Loliondo walikuwa panzi si nzige.

Amebainisha kuwa Serikali imeandaa lita 7,000 za viuatilifu vya kuua nzige hao kwa kutumia ndege ambazo watazikodi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) na shirika la kimataifa la kukabiliana na nzige.

Aliwataka wananchi na wadau wa kilimo kutoa taarifa ikiwa watabaini viashiria vya nzige katika maeneo yao.
Hao watakuwa waameenda kupanda Kilimanjaro kwa upande wasiopita watu.

Hivi zile drones za Lugola hakuna hata za samples zisaidie kuwatafuta?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom