RC Kilimanjaro aagizwa kusitisha uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU)

kirerenya Kuuza mali ya Chama cha ushirika ni uamuzi unaotakiwa kufanywa na mkutano mkuu wa ushirika. Benki ya KCBL mbali na kuwa KNCU ina hisa 68%- ambayo ndiyo mbia mkubwa haiwezi ku- dispose asset ili kuokoa biashara ambayo haijawahi kuuingiza faida tangu kuanzishwa kwake. Kwa mazingira yaliopo sasa hivi kwenye biashara ya mabenki hata wakiuza hilo shamba ili kukidhi kiwango hicho cha mtaji unaotakiwa na BOT ni ngumu sana kushindana sokoni, kwa hiyo uwezekano wa kuanguka ni mkubwa. Hilo shamba afadhali libakie mikononi mwa Chama na baadaye linaweza kuendelezwa likawa na manufaa kuliko kuuzwa ili kwenda kuokoa biashara ya hasara
Kweli kabisa mkuu.benk haijaeeza hata kuongeza branch ya pili toka ianzishwe miaka mia moja sasa. Mi naona wacha ife tu
 
Uamuzi wa PM uheshimiwe, nahisi ameshanusa UVUNDO mkubwa ktk KNCU na benki hii. tena upo mwingi sana kwa uongozi huu uliopo. Nawahakikishia mtakuja gundua hata haya mashamba walitaka kujiuzia wenyewe! Tunawajua A-Z
 
Ku
Kweli kabisa mkuu.benk haijaeeza hata kuongeza branch ya pili toka ianzishwe miaka mia moja sasa. Mi naona wacha ife tu
kuna michezo michafu sana ndani ya hii benki, ichunguzwe hasa mikopo inayodaiwa kutolewa na hailipwi walipewa akina nani! Ni wao kwa wao.
 
Mkuu wa mkoa, fuatilia kuna siri kubea hapo ofisini kwako, kwani Fedha za KCBL mwaka 2015, zienda kutumika songea. ova
 
Kila mahali ni vululuvululu....

Wataalam wetu pale hazina wanatuambia hivi ndivyo viashiria vya kasi ya ukuaji uchumi.
Wewe kila kitu sio siasa, haya ni mambo ya kisheria zaidi.
Tatizo lenu wapinga nabadiliko hampambanuwi mambo, Bali kubeza kila msichokipenda ndani ya nafsi zenu, kwa mgongo wa freedom of speech.
Ebu tuliza hilo bichwa lako na ujiulize.
Kama benki iko chini ya ukaguzi wa mdhamini wa B.O.T na pia serikali inakagua ili kujua chanzo cha Benki husika kufikia katika hali ya kufilisika,ikizingatiwa kwamba kwenye benki hiyo wanahisa wakuu ni wanachama wa ushirika husika na mwisho wa siku watahitaji kupewa taarifa rasmi ya Mali zao na nini kilitokea na kama ni nakosa ya kiuongozi na kuna hatua za kisheria zinahitajika kufuatiliwa endapo kuna ufisadi Fulani mahala fulani.

Lakini wakati hayo yakiendelea wachunguzwa hao hao wanakimbilia kuuza Mali za ushirika ili kuziba pengo la fedha,what next?
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bibi Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya kuiwezesha benki yake ya KCBL kutimiza sharti la mtaji la Benku Kuu ya Tanzania (BoT).

Benki hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili unaotosha wa shilingi bilioni tano (5) katika kipindi cha miezi sita tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama mbalimbali vya Ushirika nchini.

Alisema Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na ubadhilifu watachukuliwa hatua.

Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo zitachukuliwa hatua.

BoT ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo ihadi kufikia Juni 30, 2018.

Chanzo: ITV
Waziri mkuu ana mamlaka gani kutengua maamuzi halali ya vikao vya KNCU?

Uhakiki wa mali una uhusiano gani na kuuza mali? Haya maamuzi ya wanasiasa kuingilia ushirika ni kikwazo cha maendeleo ya ushirika.
 
Tabia kncu mlionayo, mmezoa kuuza kila kitu,mwisho mtatuambia mnataka kuuza mlima Kilimanjaro ili kuiokoa bank isifilisike.bora ifilisike kuliko kuuza mashamba ya ushirika.bank ikifa tutaanzisha nyingine,shamba nzuri na kubea hivyo tutatoa wapi jingine? Nyie kncu Ni sasa na mchwa.mchana mwema
 
Crap!!!

Kwa akili zako katika post yangu kuna sehemu nimezungumzia Siasa? Kuna sehemu nimeunga mkono mashamba ya ushirika yauzwe ili kuinua mtaji wa bank? Mi nasikitikia mabenki kufilisika we unaleta blablah za kitoto.

Hivi huko shuleni siku hizi mnaenda kusomea ujinga?
 
Waziri mkuu ana mamlaka gani kutengua maamuzi halali ya vikao vya KNCU?

Uhakiki wa mali una uhusiano gani na kuuza mali? Haya maamuzi ya wanasiasa kuingilia ushirika ni kikwazo cha maendeleo ya ushirika.
Kama PM hana mamlaka, endeleeni na mchakato WA kuuza Hilo shamba, kama hamtajikuta segerea na hakuna dhamana. Mlizoea
 
Ni kweli ni upuuzi kwa benki zilizoshindwa kujiendesha ndani ya miaka miwili ya JPM kutegemea kuwa zitafanya wonders kwa miaka yake mingine mitatu, achilia mbali ukiongeza miaka yake mingine tena mitano.
Hata hivyo, bila kupepesa macho, Agizo la PM ni sawa na kuwatangazia wateja kuwa, fedha zao ndo hivyo haziko salama na kwa bahati mbaya wateja hawaruhusiwi tena kuchota zaidi ya milioni 2 kwenye Benki hiyo.

Kwa mwenendo huu natabiri benki ndogo ndogo hizi za community, cooperatives, women etc zitakufa.

1. Wateja wameshaona ni risk kubwa ku-operate account kwenye benki hizi, kwa sababu inapotokea zinashindwa kukithi matakwa ya mtaji ya BOT wanazuia ku- draw deposits zao zote

2.
Kweli kabisa mkuu.benk haijaeeza hata kuongeza branch ya pili toka ianzishwe miaka mia moja sasa. Mi naona wacha ife tu

Na zaidi ya yote hata kama hii KCBL itakidhi kiwango cha mtaji huo wa 5 bil- utasaidia nni kuokoa vyamavya msingi vya ushirika chini ya KNCU. Kiwango hiki kinachotakiwa na BOT hata kikiwepo hakiwezi kuwa na impact yoyote ya maana.... acha ijifie tu
 
Tabia kncu mlionayo, mmezoa kuuza kila kitu,mwisho mtatuambia mnataka kuuza mlima Kilimanjaro ili kuiokoa bank isifilisike.bora ifilisike kuliko kuuza mashamba ya ushirika.bank ikifa tutaanzisha nyingine,shamba nzuri na kubea hivyo tutatoa wapi jingine? Nyie kncu Ni sasa na mchwa.mchana mwema
Wenzako wa KNCU wanataka kufunika mashimo yaliyochimbwa, ili KNCU isionekane kama kulikuwa na ubadhirifu, PM kawastukia, hakuna kuuza mali, Auditing inakuja ijulikane mapato na matumizi yametumika kivipi pale...Hahahahaha..
Lazima watu waende jela tu..
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bibi Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya kuiwezesha benki yake ya KCBL kutimiza sharti la mtaji la Benku Kuu ya Tanzania (BoT).

Benki hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili unaotosha wa shilingi bilioni tano (5) katika kipindi cha miezi sita tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama mbalimbali vya Ushirika nchini.

Alisema Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na ubadhilifu watachukuliwa hatua.

Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo zitachukuliwa hatua.

BoT ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo ihadi kufikia Juni 30, 2018.

Chanzo: ITV

Tuseme leo KCBL wamepata hizo 5 bilioni zinazotakiwa kama minimum requirement na BOT- watafanya nini?
- ndiyo wataweza kutoa mikopo kwa vyama vya msingi vya ushirika
- wataweza kupambana na ushindani wa commercial banks zilizopo
ACHA wafe lakini wateja warudishie deposits zao
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom